WAZIRI WA ELIMU, SHUKURU KAWAMBWA AKABIDHIWA FEDHA ZA MADAWATI KUTOKA TIGO
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dkt. Shukuru Kawambwa (kushoto)
akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya Shilingi 26,000,000 kwa
mwakilishi wa Hassan Maajar Trust (HMT) na Andrew Hogson, Kaimu Meneja Mkuu
wa tiGo akishuhudia. Fedha hizo zitatumika kununulia na kugawa madawati
katika shule tano kutoka wilaya za Makete na Njombe. Shule zitakazonufaika
ni Maendeleo (135), Umoja (196), Kumbila (200), Makonde (152) na Mbela (37).
No comments:
Post a Comment