EXCLUSIVE INTRERVIEW: MBUNIFU WA MAVAZI GABRIEL MOLLEL AASA KUWA WASIPOSHIRIKIANA WATAANGUSHA TASNIA YA UBUNIFU WA MAVAZI TANZANIA.
Mo Blog: Wewe ni mbunifu mwenye jina kubwa hapa nchini na nje ya nchi hii ulianza lini?
Grabriel
Mollel: Mimi naitwa Grabriel Mollel ni mbunifu wa mavazi ninamiliki
Kampuni inaitwa Sairiamu Design ambayo nimeanzisha kutoka mwaka 2009.
Mo Blog: Nini mafanikio yako tangu uingie kwenye fani hii ya ubinifu.?
Grabriel
Mollel: Unajua mafanikio sio kuwa na hela benki ila unaangalia umetoka
wapi na uliowakuta wamefanya nini na wewe umefika wapi..! Kwa sababu ni
mwaka 2010 tu nilifanikiwa kuingia katika Maonesho ya Swahili Fashion
ambayo kwangu nahesabu kama ni moja ya mafanikio yangu.
Mwaka
2011 nilifanikiwa kwenda Angola ambapo Swahili Fashion walinichagua
tukiwa na Mustafa Hassanali, lakini vile vile Millen Magesse alitufanya
sisi tukawa wageni maalum katika onesho la African Fashion Week la
Afrika Kusini ambapo hapo nilijifunza mambo mengi sana.
2012
mwezi wa tatu nilifanikiwa kwenda Kampala ambapo mimi mwenyewe ndio
nilikuwa ‘Main Designer’, kwa sababu ma-designer wengine walionyesha
nguo 10 lakini mimi nilionyesha nguo 25, ikiwemo nguo moja wa ‘Ufukweni’
(Beach wear) ambapo kwa namna nilivyoibuni hapa Tanzania huwezi
kuonyesha lakini Uganda unaweza ndio maana nikaenda kufanya ‘launch’
kule Kampala.
Pia
sasa hivi nina ofisi tatu, mbili ziko eneo la Makumbusho, moja wapo
ikiwa ni ofisi yangu binafsi, na nyingine inahusika na uzalishaji na
bidhaa zangu wako watu ambao wanatembeza jioni na pia nina wateja wa
nje.
Tangu
2003 nimekuwa nikimiliki ofisi ambayo iko Slipway japo ni gharama
lakini siku zote ukitaka kupata fedha inabidi utumie fedha. Lakini ofisi
yangu kwa pale inajulikana kama Masai Art Shop lakini iko chini ya
Brand ya Sairiamu Designs.
Mo Blog: Unatengeneza bidhaa za aina gani na wateja wako wa nje uliwapataje.
Grabriel
Mollel: Mini natengeneza mavazi na pia ‘Sandals’ na wateja wangu wa nje
niliwapata kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook. Natengeneza na
Vidani, herein na bangili za mikononi. Pia nakodisha nguo kwa sababu
nguo zangu ninazobuni ni tofauti sana kwa sababu nime-base sana kwenye
mambo ya asili. Ni nguo ambazo zinavaliwa katika shughuli muhimu muhimu
sio ya kuva barabarani.
Mo Blog: Baada ya kupata mafanikio umeweza kuisaidia vipi jamiii ya watu ulikotoka?
Grabriel
Mollel: Nilipopata mafanikio nikafikiria nilikotoka kuna ukame,
nikafikiria mradi na nimefanikiwa kuleta maji kijijini kwa kutumia
marafiki niliokutana nao kutokana na kazi hii ninayoifanya.
Mradi
huo kwa sasa unanufaisha watu 4,000 kijijini, na sasa hivi tunategemea
kuwapeleka wasichana wawili hospitali ya Mbweni . Wao watasoma kozi
fupi na wakimaliza watarudi kijijini kusaidia kwa sababu kijijini kwetu
hakuna hospitali nyingi wala wataalam.
Gharama
hizo zinabebwa na Shirika Lisilo la Kiserikali lililopo chini yangu
mimi kama Mwenyekiti na linaitwa ‘The Sairiamo Community Action
Foundation’ ambayo nimeisajili mwezi wa pili na tunategemea ‘funds’
kutoka Italia.
Mo Blog: Nini matarajio ya Ngo yako baada ya wasichana hao kuhitimu?
Grabriel
Mollel: Baada ya kuwarudisha wale wasichana kijijini tuna mikakati ya
kujenga zahanati kijijini. Kule hakuna zahanati karibu. Kwa sababu
zamani wanawake walikuwa wanatembea kilometa 18 kupata maji, bado
wanatembea kilometa 18 kufuata zahanati. Kwa vipi utamfikisha huyu
mgonjwa hospitali?
Mo Blog: Tuzungumzie ‘bifu’ baina ya wabunifu zipo kweli na kama zipo nini tatizo?
Gabriel
Mollel: Kusema kweli bifu zipo lakini kwa mimi naona ni kutokana na
watu kuzidiana uwezo, pia kutaka kuzibiana riziki na pia kingine katika
tasnia hii kuna unafiki.
Mo blog: Gabriel Joseph unaposema unafiki tufafanulie hapo.
Gabriel
Mollel: Ninamaanisha kwamba kuna watu wengine unafanyanao kazi na
wanakuchekea lakini moyoni kwao hawako na wewe kabisa, na kwa sasa hali
ni mbaya kwa sababu imengia na hata kwa ma-models.
Moja ya Ubunifu wa Gabriel Mollel.
Mo Blog: Kivipi?
Gabriel
Mollel: Usipomchagua Fulani kuonyesha mavazi katika show yako itakuwa
maneno, lakini kusema ukweli kama mimi naangalia aina ya nguo yangu
niliobuni na je? Itafaa kuvaliwa na mwanamitindo mwenye umbo gani, sasa
kama haeundani na design yangu nifanyeje? Nikuchague tu ili
nikufurahishe halafu mimi ni-fell katika kazi yangui?
Kingine
pia waandishi hawako makini na kazi zao, wanaandika bila ya kuthibisha
habari wanazoziandika, huwa zinachangia kutuvuruga wabunifu.
Mo Blog: Nini Ushauri kwa wabunifu wenzako?
Gabriel
Mollel: Kuna watu wanatishiana ubaya, nawashauri sio kitu kizuri na
pia tujenge utamaduni wa kusaidiana aliyeko juu amnyanyue anayechipukia.
Model na Vazi la Ubunifu wa Gabriel Mollel.
Mo Blog: Mbunifu gani wa mavazi hapa nchini ambaye kwako unampa ‘Big Up’ ?
Gabriel Mollel: Kwa kweli namuamini sana Daiana Magesa, na Manju Msita namheshimu kwa ubunifu wake.
Mo Blog: Tuambie umewahi kupata tuzo yeyote katika shughuli zako hizi za ubunifu wa mavazi?
Gabriel Mollel: Ndio nimewa kupata tuzo kama ifuatavyo:-
-The Most Innovative Designer of The year – 2011
-The Best Designer of the Year -2011
-The Men Wear of The Year -2011 –Swahili Fashion Week
-Red Carpet Designer of the year
Mo Blog: Kipi kimewahi kukukera katika shughuli zako hizi.
Gabriel
Mollel: Kuna wakati Swahili Fashion week kulikuwa na mizengwe na
ubabaishaji mwingi, mambo yalikwenda ndivyo sivyo lakini yote sawa
nitaendelea na ubunifu wangu wa kutumia vitu vya asili.
Mo Blog: Neno la mwisho kwa tasnia ya ubunifu.
Gabriel
Mollel: Asanteni sana Mo Blog kwa kuja kuzungumza na mtu kama mimi
naombeni muendelee kuwatembelea wabunifu wengine wa mavazi, kingine kwa
wabunifu wenzangu tuwezeshane, tushirikiane na tushikamane ili kukuza
fani hii, mwisho kabisa tusikatishane tamaa kwa sababu wako baadhi ya
watu ukitaka kuanza ubunifu wanakukatisha tamaa na kukukandamiza chini.
Nawaambia hayo sio maadili ya ubunifu, ukiona mtu anajaribu msaidie.
Mo
Blog:Gabriel Mollel sisi wana Mo Blog tunakutakia mafanikio mema na
uweze kuzitangaza bidhaa zako za kiasili kwa wingi nje ya nchi kwani
utakuwa umeitangaza Tanzania kwa ujumla.
Gabriel Mollel: Akhsanteni sana nawakaribisha watanzania wote kuangalia bidhaa zangu katika maduka yangu na Mungu awabariki.
“I WILL REACH FAR; I KNOW WHAT I AM DOING BECAUSE I HAVE STARTED FROM SCRATCH.”
Mahojiano na: Lemmy Hipolte na Gabriel Joseph.
Picha na : Jofrey Mwakibete.
Msimamizi: Zainul Mzige. (kwa hisani ya Mo blog)
No comments:
Post a Comment