Ikiwa ni siku tisa tu toka
kutokea kwa ajali ya Mv Skagit iliyochukua maisha ya Watanzania zaidi ya
80, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali
Mohamed Shein ameiagiza Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais, Fedha, Uchumi na
mipango ya maendeleo kuandaa utaratibu wa kupata fedha ndani ya wiki
moja kutoka sasa kwa ajili ya kununua meli kubwa mpya ya abiria elfu
moja na yenye uwezo wa kubeba mizigo ya tani 100.
Ametoa hilo agizo wakati
akizungumza na uongozi wa shirika la meli pamoja na wajumbe wa bodi ya
shirika hilo ambapo ameagiza wizara kutafuta hizo pesa kutoka kwa
vianzio vya ndani au nje ya Nchi vilevile taasisi zinazohusiana na mambo
ya fedha.
Dr Shein amesema katika kipindi
kisichozidi miezi miwili anahitaji ujumbe maalum uende kwenye kampuni
zinazotengeneza meli Korea Kusini, China au Japan kwa ajili ya
kuwasilisha fedha za utangulizi kwa ajili ya ujenzi wa hiyo meli.
Baada ya kusema hayo, Uongozi
wa shirika la Meli ulimueleza kwamba kwa kawaida ujenzi wa meli yenye
ukubwa huo huchukua mwaka mmoja kukamilika.
Kikao hicho kilikua na lengo la
kuangalia mwelekeo na mipango ya shirika la meli pia, kilijadili hali
ya meli za shirika la meli na baadae kujadili masuala ya ununuzi wa meli
mpya itakayoondoa usumbufu wa usafiri wa baharini wananchi wanaosafiri
kati ya Unguja, Pemba na Tanzania bara.
No comments:
Post a Comment