Wabunge wamsafishia Zitto njia ya Urais 2015!
IKIWA
imebaki miaka mitatu kabla ya Uchaguzi Mkuu utakaofanyika nchini mwaka
2015, wabunge wawili vijana wamewataka wakazi wa Mkoa wa Kigoma
kujiandaa kumpata kutoka eneo hilo.
Kauli
za Wabunge hao zimekuja kipindi ambacho mchakato wa Katiba unaendelea
huku kukiwa na uwezekano wa umri wakugombea urais kushuka hivyo
kuwawezesha wanasiasa wengi vijana akiwamo Zitto, kugombea nafasi hiyo.
Wakizungumza
katika tamasha kubwa lililokutanisha mamia ya wakazi wa Mkoa wa
Kigoma, Deo Filikunjombe ambaye ni mbunge wa Ludewa (CCM), Joshua
Nasari wa Arumeru Mashariki (Chadema) na Halima Mdee, Kawe (Chadema),
walisema wanaamini Rais wa 2015 atakuwa Mbunge wa Kigoma kaskazini na
ambaye ni mzaliwa wa mkoa huo.
Katika
kauli yao hiyo, wabunge hao walisema Mbunge huyo ameonyesha umahiri
mkubwa katika kusimamia mambo ya kitaifa bila upendeleo, jambo
linalomfanya kujijengea umaarufu mkubwa ndani na nje ya nchi, hivyo
kuonekana wazi kulibeba vema kundi la Vijana wa Taifa hili.
Akimzungumzia
kuhusu rais ajaye kutoka Kigoma, Filikunjombe alisema kundi la vijana
lazima liungane kuhakikisha kuwa linatoa viongozi watakaopigania
maslahi yao na Taifa kwa jumla ili kuleta ukombozi wa kifikra na
kimaendeleo kwa maslahi ya jamii.
"Lazima
mtambue kuwa, Tanzania ni nchi yetu sisi wote na lazima vijana wote
bila kujali itikadi zetu za kisiasa tunatakiwa kujipa moyo kwamba
tunaweza kufanya makubwa katika kuleta maendeleo ya jamii katika nchi
yetu," alisema Filikunjombe na kuongeza:
"Vijana
wa Kigoma mnabahati ya kuwa na Wabunge wazuri na ninaamini miaka
michache ijayo lazima mkoa huu utoe Rais wa Tanzania."
Huku
akishangiliwa na umati mkubwa wa watu waliokusanyika katika uwanja wa
Lake Tanganyika mjini hapa kuhudhuria tamasha hilo lililopambwa na
wasanii nyota wa kizazi kipya kutoka Mkoa wa Kigoma, Filikunjombe
alisema; "Zitto anastahili kuwa rais".
Mbunge
huyo wa CCM ambaye katika siku za karibuni ameonekana kuwa mshirika
mkubwa wa kisiasa wa Zitto na Chadema, alisema Zitto anafaa kuwa Rais
kwani amefanikiwa kuwaunganisha watu na kuleta umoja miongoni mwao,
jambo ambalo linadumisha umoja wa kitaifa.
Kauli ya Nassari
Kwa
upande wake Nasari, alisema Mkoa wa Kigoma umejitokeza wazi kuwa na
wanasiasa mahiri na wenye vipaji vya hali ya juu katika kupigania
maslahi ya wananchi pamoja na kupambana na ufisadi unaodidimiza uchumi
wa taifa letu na kuwanufaisha wachache kwa kutumia nafasi zao.
‘Leo,
ni mara yangu ya kwanza kufika Kigoma, lakini kwa jinsi ninavyoona
mpangilio mzuri wa shughuli hii, naamini kabisa kuwa, Zitto Kabwe
aliyeandaa hafla hii na kuwakusanya wasanii wa Kigoma kuwa kitu kimoja
anafaa kabisa kuwa rais ajaye wa Taifa letu. Na haya ninayasema kwa
uhakika bila hata chembe ya mzaha," alisema Nasari.
Huku
akishangiliwa na mamia hayo ya wakazi wa Kigoma, alifafanua kwamba
wanasiasa vijana wamejipanga kuwatetea wananchi na hususani kundi la
vijana katika kuondoa matatizo mbalimbali yanayowasibu katika maisha kwa
kuwajengea mazingira mazuri ya kufanya kazi zao za uzalishaji mali.
Mdee amliza Zitto Katika
hatua nyingine, Mbunge wa Kawe Halima Mdee (Chadema) alimliza Zitto
jukwaani baada ya kumuelezea kuwa ni ‘jembe’ katika mambo mbalimbali na
mtu mwenye uchungu na maendeleo ya taifa.
Mdee
aliyepewa nafasi ya kuwasalimia Wananchi alisema amekuwa na Zitto
tangu Chuo kikuu cha Dar es Salaam na kwamba kutokana na ujasiri na
umahiri wake katuika kutetea masilahi ya wanyonge na taifa, anafaa kuwa
mmoja wa viongozi wa juu katika Taifa.
‘Ndugu
zangu watu wa Kigoma, kwa kweli mna bahati sana, achilia mbali kuwa na
vipaji katika sanaa ya muziki na michezo hasa mpira wa miguu, lakini
mna wanasiasa wakali ambao ni tishio hapa nchini. Mimi namkubali sana
Zitto Kabwe na ninaamini kuna siku atakuwa kiongozi wa juu katika nchi
yetu," alisema Mdee.
Mdee alipongeza ushirikiano wa wananchi wa Kigoma na kusisitiza kuwa unatakiwa kuenziwa na kuigwa na mikoa mingine.
Zitto akiri kutoa machozi
Zitto
alipulizwa na gazeti hili alikiri kudondosha machozi jukwaani kutokana
na Mdee kuzungumza kwa hisia kali na hivyo maneno yake kumchoma na
kushindwa kujizuia jukwaani.
"
Kwa weli Halima Mdee aluzumgumza maneno mazito sana na alinikumbusha
mbali enzi za Chuo kikuu tukiwa kwenye harakati za kutetea maslahi ya
wanachuo na pia nimekuwa naye kwenye harakati za kisiasa ndani ya
Chadema, ndiyo maana nilishindwa kujizuia na kuanza kutoa machozi,"
alisema Zitto.
Alisema
amefarijika kuwaona wabunge wenzake kutoka vyama vya CCM, NCCR
Mageuzi, Chadema na CUF wamefika Kigoma kumuunga mkono katika uzinduzi
wa wimbo wa 'Leka dutigite' ulioimbwa kwa pamoja na wasanii wa muziki
wenye asili ya Kigoma.
Zitto
alisema Mkoa wa Kigoma kwa muda mrefu umekuwa nyuma kimaendeleo hivyo,
kuufanya kudharauliwa na watu wengi hata kama hawajui lolote juu ya
eneo hilo.
‘Wapo
watu wanaotubeza kwamba mkoa wetu ni masikini na haufai kuishi, na
kasumba hii imejengeka hadi kwa baadhi ya watumishi wa Serikali. Ndiyo
maana sishangai ninaposikia kwamba kuna watumishi wa Serikali wanakataa
kuhamia Kigoma. Lakini hii dhana sasa itaisha," alifafanua Zitto.
Wabunge waliohudhuria
Wabunge
waliofika Kigoma kwenye hafla hiyo ni Mdee , Amina Mwidau wa viti
maalumu (CUF), Esta Bulaya ( Viti maalumu (CCM), Filikunjombe (CCM),
Kangi Lugola wa Mwibara, David Kafulila (Kigoma Kusini, NCCR-Mageuzi),
Nasari (Arumeru Mashariki Chadema) na Raya Ibrahim Khamis wa viti
maalumu kutoka Pemba.
Kauli ya Nape
Alipoulizwa
Katibu Mwenezi wa CCM Nape Nnauye kuhusu Filikunjombe kumtabiria Zitto
kuwa Rais wakati anatoka upinzani, alisema hawezi kuzungumzia suala
hilo kwa kuwa hajasikia wala kulisoma popote.
“Nyie
andikeni kwanza halafu ndiyo nitaweza kusema, kwa sasa siwezi kusema
chochote kwa sababu sijasikia kitu chochote ama kusoma popote pale jambo
hilo,” alisema Nape.
Credit kwa mwananchi
No comments:
Post a Comment