Thursday, July 26, 2012

TAFAKARI CHUKUA HATUA:::::MTANZANIA MWENZANGU HII NDIO TUNAIITA HOSPITALI YETU KUU YA TAIFA KWELI?HEBU TAZAMA WATU WANALALA CHINI TENA KORIDONI BILA HATA GODORO?

Hii ndio hali ilivyo katika wodi za Muhimbili, pamoja na serkali kudai huduma kurejea kama kawaida.Waandishi wa habari wanaweza kwenda kuwahoji wagonjwa wodi za SewaHaji ground floor.

  Haya ndi mazingira ya Hospital yetu kuu Tanzania, watu wanalala chini kwenye korido, wengine bila hata magodoro, sasa wakina Dr Ulimboka walipokua wanasema mbali na posho zao kuongezwa wanataka mazingira mazuri ya kazi mkawaona wanajipendelea, mazingira mazuri ya kazi ya dr ni kuona mgonjwa wake analala sehemu nzuri na safi, sio chini. But wengi wenu mmekua mkidhani madr wanajipendelea tu. Katika hospital kuu kama hii hadi mama mjamzito anaambiwa aje na gloves zake sijui pamba zake yaani serikali inashindwa kweli kuwapa wananchi vitu muhimu kama hivyo? na kila kukicha watu flani flani kuutwa wako ma-airport na umati wa waapambe, kweli Madr wataacha kugoma hapo?  

Ingawa Serikali inadai wauguzi wamerudi kazini ila bado kunaonekana kama kuna mgomo baridi unaoendelea, wauguzi wote wanaonekana kutofurahishwa na mazingira ya kazi ila ndio hivyo tena hawana jinsi...baba riz1 amezidi kuwa m-babe watu wameona isiwe tabu, ila we baba ujue ubabe sio dili wala nini, mtu akiomba haki yake na asikilizwe na sio kupigwa mkwara.


But, anyway, who am i for you to listen to me? na ndio maana people can not WAIT for 2015 angalu tuone CHANGES jamani, it such a shame kwa kweli, we umeona wapi hospital kulivyokua na magonjwa ya kila aina mtu analala chini tena jamani??? mweeh kweli vitu vingine vinatokea Tanzania tu !!! siamini km serikali inashindwa kuchongesha vitanda jamani, vitanda tuuu??? au navyo tunategemea mpaka tupewe misaada? hatuna mbao nini?
                         Picha na Jamii Forums

No comments:

Post a Comment