BAADA YA MV SKAGIT, HII NDIO TAARIFA RASMI YA AJALI NYINGINE YA JANA.
kama unakumbuka wakati MV SPICE
ISLANDERS inazama muda mfupi baadae kuna jahazi la mizigo lilizama
likitokea Tanga, sasa stori ya leo ni kwamba baada ya MV SKAGIT kuzama
wiki iliyopita Jeshi la Polisi Zanzibar limethibitisha kuzama kwa Jahazi
jumatano ya July 25 2012 siku saba baada ya ajali ya MV SKAGIT.
Msemaji wa Polisi Mohamed
Mpinga ameiambia millardayo.com kwamba Jahazi lilikua linatokea Kusini
Pemba kwenda Nungwi kaskazini Unguja ambapo mtoto wa miaka mitano Isaka
Hamis alipoteza maisha.
Polisi mkoa wa Kusini Pemba wamesema chanzo cha ajali ni ujazaji wa mizigo uliopitiliza kwani Jahazi hilo lilibeba magunia kumi ya Muhogo, mikungu 10 ya ndizi pamoja na mizigo mingine ya kuni.
Watu sita walinusurika kifo
akiwemo mama mwenye mtoto wa miaka miwili, vyombo hivi vya uvuvi vimekua
vikitumika kusafirisha abiria na mizigo kimakosa wakati pia havitakiwi
kusafiri umbali mrefu.
No comments:
Post a Comment