Inawezekana stori nyingine huwa unazichukulia poa, lakini hii usiichukulie poa hata kidogo.
Ninachotaka kukwambia ni kwamba aina ya ugonjwa wa ukimwi ambao hausikii dawa umekua ukiongozeka kwenye hili bara la Afrika katika muda wa muongo mmoja uliopita.
Ninachotaka kukwambia ni kwamba aina ya ugonjwa wa ukimwi ambao hausikii dawa umekua ukiongozeka kwenye hili bara la Afrika katika muda wa muongo mmoja uliopita.
BBC wamesema, kuna ripoti ilimeandikwa na wataalam kwenye jarida la kisayansi la Lancet.
Wataalamu hao wamesema hali
hiyo ya ugonjwa kutosikia dawa huenda ikatokea ikiwa wagonjwa hawata
zingatia na kutumia dawa walizopewa na pia ufuatiliaji mbaya.
Hali hiyo inazusha hofu zaidi
katika bara la Afrika ambako hakuna njia mbadala ya kuwatibu wanaouguwa
maradhi ya Ukimwi ambapo watatifi kutoka shirika la Afya duniani-WHO na
chuo kikuu London wamegundua kwamba aina ya ukimiwi ambao hausikii dawa
unapatikana zaidi kwenye nchi za Afrika Mashariki.
Yani wanasema asilimia 26% ya
waathirika wako katika hali hiyo ikilinganishwa na asilimia 14 katika
nchi zilizo kusini mwa Afrika, Lakini kwenye nchi za Amerika, Afrika Magharibi na kati hakuna kitu kama hicho.
Chanzo kikubwa cha hayo yote ni
kwa sababu wagonjwa hawatumii dawa kama inavyotakiwa ambapo hii stori
imetoka siku tano tu baada ya kumsikia waziri mkuu Mizengo Pinda akisema
Tanzania imekua miongoni mwa nchi 36 duniani zilizofanikiwa kupunguza
maambukizi mapya ya UKIMWI kwa asilimia 25.
No comments:
Post a Comment