Thursday, July 26, 2012

ZIARA YA NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI MHE. DKT. CHARLES TIZEBA (MB) KATIKA BANDARI YA DAR ES SALAAM JANA


Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt. Charles Tizeba akifafanua jambo kwa uongozi wa Wizara, Bandari na Mkurugenzi Mtendaji wa Kitengo cha Kupakia na kupakua makontena TICTS, kulia kwa Naibu Waziri ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Bw. John Mngodo, Kushoto kwa Naibu Waziri ni Meneja Msaidizi wa Bandari ya Dar es Salaam, Bi Winnie Mulindwa, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo(aliyevaa tai ya blue), Mhandisi Omar Chambo, na Kulia kwa Katibu Mkuu ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Kupakua na Kupakia Makontena (TICTS), Bw. Neville Bisett.
 
Naibu Waziri wa Uchukuzi,Dkt. Charles Tizeba (Mb),akiongea na baadhi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania(hawapo pichani),wakati alipotembelea Taasisi hiyo leo jijini Dar es Salaam,Kushoto kwa Naibu Waziri ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Mhandisi Omar Chambo, Naibu katibu Mkuu wa Wizara hiyo (wa pili kushoto),Bw. John Mngodo. Na aliyevaa Kizibao ni Meneja Msaidizi wa Bandari ya Dar es Salaam,Bi. Winnie Mulindwa.
 
Meneja Msaidizi wa Bandari ya Dar es Salaam, Bi. Winnie Mulindwa, akitoa taarifa ya namna Bandari ya Dar es Salaam inavyofanya kazi kwa Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Charles Tizeba (aliyeshika kichwa), ambaye amefanya ziara ya siku moja katika Bandari ya Dar es salaam. Kushoto kwa Naibu Waziri ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Mhandisi Omar Chambo, Kulia kwa Katibu Mkuu ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo,Bw. John Mngodo, Kushoto kwa Meneja Bandari Msaidizi ni Mkurugenzi wa Idara ya Usalama na Mazingira kutoka Wizara ya Uchukuzi,Bi. Tumpe Mwaijande.
 
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya kupakua na kupakia makontena Bandarini (TICTS), Bw. Neville Bisett akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Charles Tizeba (Mwenye Suti ya Mikono Mifupi),wakati alipofanya ziara ya siku moja kuangalia ufanisi wa Kampuni hiyo katika Bandari ya Dar es Salaam leo.Kulia kwa Naibu Waziri ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi,Bw. John Mngodo.(Picha Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Uchukuzi).

No comments:

Post a Comment