BREAKING NEWSSSSSSSSSSSSSS WATU WAPIGA WALI NA KUSHUSHIA NA KINYWAJI CHA
TOGWA AMBACHO KIMEPELEKEA KUUA MTU MMOJA NA KUFUATIA 40 HOI JIJINI
IRINGA!
Wahanga wa tukio hilo wakiwa hoi kituo cha afya Ipogolo Iringa
Mganga mfawidhi wa kituo cha afya Ipogolo Dkt mary Makundi
Mwenyekiti
wa serikali ya kijiji cha Ibofye wilaya ya Kilolo Godfrey Mtete
(kushoto) akiwa na mgonjwa mwingine ktk kituo cha afya Ipogolo
walikolazwa kwa kula chakula chenye sumu
MTU mmoja mkazi wa kijiji cha
Ibofye wilaya ya Kilolo mkoani Iringa amefariki dunia na wengine
zaidi ya 40 wamelazwa katika Hospitali mbali mbali za mkoa wa
Iringa kikiwemo kituo cha afya Ipogolo na Hospital ya rufaa ya
mkoa wa Iringa baada ya kula wali na kunywa togwa zinazosadikika
kuwa na sumu katika shehere ya kutoa mahali .
Wahanga wa tukio hilo ambao wamelazwa katika kituo cha afya cha
Ipogolo mjini Iringa waliueleza mtandao huu wa
www.francisgodwin.blogspot.com leo kuwa tukio hilo lilitokea juzi
jumamosi baada ya mkazi wa kijiji hicho Bw James Ngaile kuandaa
chakula na kinywaji hicho aina ya togwa kwa kwa ajili ya sherehe ya
kuoza binti yake.
Alisema Yamile Mhehe ambaye amelazwa katika kituo hicho cha afya
kuwa utaratibu wa chakula katika sherehe hiyo ilikuwa ni sahani
moja kwa watu watatu na kuwa chakula kilichoandaliwa ni wali na
ugali huku mboga ikiwa ni maharage na kabichi na baada ya chakula
wageni walikuwa wakitumia kinywaji aina ya togwa kwa ajili ya
kushushia chakula hicho.
Hata hivyo alisema baada ya kula chakula hicho muda wa saa moja
usiku wananchi waliofika katika sherehe hizo walitawanyika kurejea
majumbani kwao na kuwaacha walengwa wa sherehe hiyo wakiendelea na
mapumziko ya usiku.
Alisema baada ya kufika nyumbani muda wa saa 2 usiku tumbo la
kuharisha damu lilianza kumsumbua yeye na mke wake na hivyo
kulazimika kukimbia kwa majirani kuomba msaada zaidi na baada ya
kufika huku walikuta majirani zao nao wakisumbuliwa kama wao hali
iliyowalazimu kutoa taarifa kwa mwenyekiti wa kijiji ambaye pia
alikuwa hajiwezi kutokana na kukumbwa na tatizo kama hilo.
Hivyo kutokana na hali hiyo kuonekana kuwakumba watu zaidi ya 20
katika kijiji hicho uongozi wa kijiji ulilazimika kukodisha
daladala na kuwachukua wagonjwa wote na kuwapeleka kituo cha afya
Ihimbo na baadhi yao ambao hali zao zilionekana kuwa mbaya
walikimbizwa kituo cha afya Ipogolo na wengine Hospital ya Rufaa ya
mkoa wa Iringa.
Mwenyekiti wa serikali ya kijiji hicho Godfrey Mtete alisema kuwa
tukio hilo ni la kwanza kutokea katika kijiji hicho na kuwa hadi
sasa bado hawajabaini tatizo lilikuwa katika chakula ,mboga ama
togwa hiyo kwani alisema mbali ya tatizo hilo kuwakumba watu
waliofika katika sherehe hiyo baadhi ya watoto kama watatu
wamelazwa patwa na mkasa huo japo hawakula chakula wala kunywa
kinywaji katika sherehe hiyo.
Mtete alisema hadi sasa mtu mmoja ambaye yeye alikuwa akimwita
mjombe wake aliyemtaja kwa jina la Wagila Nyaupumba amefariki dunia
kabla ya kukimbizwa hospital kwa matibabu.
Mwenyekiti huyo alisema kuwa idadi ya wananchi waliopatwa na tatizo
hilo ni 40 na kuwa watu zaidi ya 38 ndio ambao walionekana kuwa
mahututi zaidi na kukimbizwa kupatiwa matibabu huku baadhi ya
wananchi wameendelea kufikishwa Hospitalin jana baada ya kuonekana
kuathirika na chakula hicho.
Alisema hatua ambayo kijiji kimechukua kuhusu chakula hicho ni
kuzuia chakula hicho kumwagwa wala kupewa nguruwe ili kiweze
kuchunguzwa zaidi .
Aidha alisema mbali ya chakula hicho kuwakumba wageni waliofika
katika shughuli hiyo ya kuona binti bado bibi harusi mtarajiwa na bwana
harusi pamoja na wazazi wa pande zote mbili pia ni wahanga wa
tukio hilo .
Mganga mfadhiwa wa kituo cha afya Ipogolo Dkt Mary Makundi
alithibitisha kupokea wagonjwa 9 kati ya 40 katika kituo hicho na
kuwataja wagonjwa waliolazwa katika kituo hicho kuwa ni Rafiki
Kabogo, Beth Ngaile, Neema Ngaile, Emelia Mwalafi, Edina Mkemangwa,
Costanzia Maliga, Ayubu Kaywanga Godfrey Mtete na Yamile Mhehe.
Huku akidai hali zao zinaendelea vizuri na kuwa wagonjwa wengine
walifikishwa hospitali ya mkoa wa Iringa na kituo cha afya Ihimbo
kwa matibabu zaidi .
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Michael kamhanda alipoulizwa
na mtandao huu kwa njia ya simu jana kuhusu tukio hilo alisema bado
halijafika ofisini kwake na kuwa pindi litakapomfikia atalitolea
ufafanuzi.
No comments:
Post a Comment