Monday, July 16, 2012

MAREHEMU CHRIS MWAMBONDA KUZIKWA LEO SAA 8 MCHANA HUKO GOBA

Mwandishi Mwandamizi wa Habari za Michezo, Chris Mwambonda aliyefariki usiku wa kuamkia jana jijini Dar es Salaam, anatarajiwa kuzikwa leo Jumatatu saa 8 mchana nyumbani kwa mama yake mzazi huko Goba. Kwa mawasiliano ya kuweza kufika na kushiriki mazishi hayo, maelekezo yatatolewa kwa yeyote atakayehitaji kufanya hayo kupitia namba ya simu: 0758 333 436. Pichani, Mwambonda kushoto katika moja ya matukio aliyoshiriki enzi za uhai wake ambapo hapa anaonekana akikabidhiwa na Mkurugenzi wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Leonard Thadeo, cheti cha ushiriki wa mafunzo yaliyowashirikisha Wahariri wa Michezo yaliyofanyika Juni 10 2010.

No comments:

Post a Comment