SUMATRA: MELI YA MV SKAGIT ILIKUWA NA ABIRIA 248, WATOTO 31 NA MABAHARIA 9
MAMLAKA ya
udhibiti usafiri wa nchi kavu na maji (SUMATRA),imesema meli ya MV
Skagit iliyopata ajali visiwani Zanzibar, iliondoka Bandari ya Dar es
Salaam saa 06.05 mchana juzi ikiwa na abiria 248, watoto 31 pamoja na
mabaharia 9.
Meli hiyo
inayomilikiwa na Kampuni ya Seagul Transport, ilipata usajili katika
Mamlaka ya usafiri Bandari Zanzibar (ZMA)ikiwa na uzito wa meli
(GRT)96.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Meneja Mawasiliano
David Mziray, alichanganua kuwa cheti cha ubora wa meli hiyo kilitolewa
Agosti mwaka jana na kumalizika mwezi huo mwaka huu.
“Mv Skagit
ilikuwa na uwezo wa kubeba abiria 300 pamoja na mizigo tani 26, hivyo
kulingana na idadi ya abiria 288 walioondoka katika chombo hicho
isingeweza kuleta madhara kama hayo, ila tunawasiwasi waliongeza abiria
njiani au mawasiliano ya hali ya hewa” Kwa mujibu wa Mziray.
Aidha,
anafafanua kuwa idadi ya watu waliopoteza maisha hadi sasa ni zaidi ya
34, majeruhi 146 wakati wengine wakiendelea kutafutwa.
“Zoezi la
uokoaji linaendelea katika eneo la tukio kwa msaada wa Mv Flying Horse,
Mv Kilimanjaro 111, Tug Bandari ya Zanzibar, KMKM, Mv Zanzibar 1, Polisi
wa majini, pamoja na Navy, hata hivyo bado taarifa sahihi za
waliopoteza maisha hazijapatikana kulingana na watu hao kuokolewa katika
mazingira tofauti” alibainisha Mziray.
Hata hivyo
alisema baadhi ya viongozi wa Sumatra wamekwenda katika tukio hilo kwa
ajili ya kushirikiana na ZMA ili kuokoa maisha ya watu hao.
No comments:
Post a Comment