KAMBI
Rasmi ya Upinzani Bungeni imeitaka serikali kutoa ufafanuzi kama kuna
mtambo ulionunuliwa kutoka nchini Israel kwenye Kampuni ya NICE maarufu
kama Gi2, ambao ni maalumu kwa ajili ya kufanya “sms spoofing”.
Taarifa hizo zinadai kuwa mtambo huo uliuzwa kwa Jeshi la Polisi nchini Aprili mwaka huu.
Kauli
hiyo ilitolewa jana na Naibu Msemaji wa kambi hiyo, Wizara ya
Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Joshua Nassari, wakati akisoma
hotuba yao.
Nassari
alisema wataalamu waliowasiliana nao na mitandao mbalimbali kama vile
www.textfromwho.com walionesha teknolojia hii ya “sms spoofing” yenye
uwezo wa kutuma ujumbe wa simu ya mkononi kwa kutumia simu ya mtu
mwingine kana kwamba ni mwenye namba ya simu aliyetuma ujumbe huo.
“Mheshimiwa
Spika chuo kimojawapo kilichopo India cha “The Asian Schools of Cyber
Laws” (Pune) walifanya utafiti juu ya jambo hili na majibu ya utafiti
huo ni kuwa waliweza kutuma ujumbe mfupi wa simu kwa kutumia njia hii na
waliweza kutumia simu za watu waliokuwa mtandao wa “GSM” kwenye mabara
ya Afrika na Asia.
“Utafiti
ulionesha kufanikiwa kutumia namba za simu za watu wengine na kutuma
ujumbe mfupi wa simu,” alisema na kuongeza kwamba vyanzo mbalimbali vya
taarifa ni kuwa mtambo kama huo unatumika kwenye nchi za Israel na
Ujerumani ila kwa nchi nyingine kama Australia kufanya tendo hilo ni
kosa kisheria kwani wao wamepiga marufuku matumizi ya mfumo huo.
Nassari
aliongeza kuwa mwaka 2008 nchini Uingereza, kampuni ya udhibiti wa
mawasiliano wa viwango vya juu inayojulikana kama “phone pay plus”
ambayo kabla ilijulikana kama ICSTIS walianzisha kanuni kwa ajili ya
wateja kuweza kutoa malalamiko kama simu zao zimefanyiwa uharamia huo.
“Kambi
ya Upinzani tunataka kupata majibu juu ya mambo yafuatayo; Je, taarifa
za mtambo huo wa Gi2 kununuliwa na kuletwa nchini na kutumiwa na Jeshi
la Polisi mwaka huu ni za kweli?” alihoji.
Msemaji
huyo alibainisha kwamba wanataka kujua mtambo huo umeletwa kwa
madhumuni gani hasa na utakuwa unatumika kwenye masuala gani.
“Mtambo
utakaonunuliwa na TCRA ni wa aina gani na utakuwa na uwezo wa kufanya
sms spoofing, na kwamba kama jibu ni ndio, zitatumika kufanyia shughuli
gani hasa,” alisema.
Kauli
ya CHADEMA inakuja siku chahe tangu, mjumbe wa Kamati Kuu na mshauri
wa chama hicho, Mabere Marando, kudai kuwa wamenasa mbinu za uwepo wa
mtambo huo na kuwa ndio ulitumika kumtumia sms za vitisho Mbunge wa
Iramba Magharibi (CCM), zikionesha kuwa zimetoka kwa wabunge wa CHADEMA.
Bil 1.3/- zaibiwa mtandaoni
Katika
hatua nyingine, kambi ya upinzani bungeni ilitaka kujua serikali
imejiandaaje ili kudhibiti uhalifu wa kimtandao unaoshika kasi.
Nassari
alisema kwa sasa kiasi kilichoripotiwa Polisi kuhusiana na wizi kwa
njia ya mtandao hapa nchini ni sh bilioni 1.3, Euro 8,897 na dola za
kimarekani 551,777.
“Uhalifu
huu wa kimtandao unaongezeka kwa kasi kubwa sana hapa nchini mwetu na
unatishia uhai wa uchumi wetu kama taifa kama hatua hazitachukuliwa
mara moja,” alisema.
Kuhusu
kubadili mfumo wa utangazaji kutoka analojia kwenda digitali, kambi ya
upinzani na Kamati ya Bunge ya Miundombinu waliitaka serikali
kuhakikisha ving’amuzi vinauzwa kwa bei ambayo Watanzania wa kawaida
wataweza kuimudu, vile vile ihakikishe king’amuzi kinakuwa kimoja chenye
kubeba vituo vyote.
Msemaji
wa kamati hiyo, Profesa Juma Kapuya alisema wanaitaka serikali kuweka
umakini katika uchimbaji wa madini ya urani utakaoanza hivi karibuni
huko Namtumbo, Bahi na Manyoni.
Tanzani Daima
No comments:
Post a Comment