Vodacom Tanzania kuwanufaisha wateja watakaonunua LUKU kupitia M-pesa
· Wateja kupata muda wa bure wa maongezi wa shilingi 1000 kila watakapo nunua Luku kupitia M- Pesa
· Kujua salio mteja atapiga *102# au *103#
Dar es Salaam 24 julai 2012..... Kampuni
ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania imezindua ofa mpya kwa wateja
wanaotumia huduma ya M-pesa kununua Luku ambapo sasa kila mteja atakae
tumia huduma hiyo atapata muda wa bure wa maongezi wa shilingi elfu 1000
bila ya kujali ni mara ngapi mteja amenunua Luku kwa siku.
Muda huo wa
maongezi ambao utadumu kwa siku mbili, mteja ataweza kuutumia kupiga
simu kutoka Vodacom kwenda Vodacom na kutuma ujumbe mfupi wa maneno
kwenda mitandao yote Tanzania.
Huduma hiyo ya
kununua Luku kupitia M – Pesa inawawezesha wateja mbalimbali kulipia na
kununua umeme mjini na vijijini na kwa urahisi. Ili wateja kujua salio
la muda huo wa bure wa maongezi, watahitajika kupiga *102# au *103#.
Akizungumza na
waandishi wa habari wakati wa uzinduzi huo, Mkurugenzi mtendaji wa
kampuni ya Vodacom Tanzania Bwana Rene Meza, amesema kuwa ofa hiyo
imelenga kuwahamasisha wateja wa Kampuni ya Vodacom kuendelea kutumia
huduma ya M-pesa kununua Luku ikiwa ni njia ya kuendelea kuboresha
huduma ya M-pesa sio tu kwa kutuma na kupokea pesa bali hata kuwawezesha
wateja kufanya malipo mbalimbali kama kulipa ada za shule kupitia
huduma hiyo.
“Ni kwa sababu
hiyo ndio maana tunawapa motisha wateja wanaotumia huduma ya M-pesa
kununua LUKU kwani tunataka waendelee kutumia huduma hii kadri wawezavyo
na hata kuhamasisha wateja wote wa Vodacom kutumia huduma hiyo” alisema
Meza huku akiongeza kuwa wale wote ambao hawajatumia huduma hiyo sasa
wanayo sababu ya kuitumia.
“Huduma hii ni
muafaka katika maisha ya sasa kwani inaokoa muda mwingi wa mazungumzo
kwa wateja wetu. Napenda kuwapa changamoto wale ambao hawatumii huduma
hii kuanza kuitumia kwani sasa tunaishi katika dunia ambayo ni muhimu
kutunza muda” alisisitiza Meza.
Ofa hii imekuja
punde tuu baada ya kampuni hiyo kuzindua ofa nyingine mapema mwezi
iliyotoa muda wa bure wa maongezi kwa wateja wanao tumia huduma ya M –
Pesa kila wanapotuma na kupokea pesa.
Kwa mujibu wa
Meza, kampuni ya Vodacom Tanzania inajivunia namna ambavyo wateja wake
wanavyoiunga mkono katika huduma mbalimbali zinazotolewa na kampuni
hiyo. Alisema kuwa Vodacom Tanzania inatambua mchango na thamani mkubwa
waliopewa na wananchi ndio maana wanawapa huduma ambazo zinakidhi
mahitaji yao ya kila siku.
Tangu kuanzishwa
kwake mwaka 2008 huduma ya M-pesa imeleta mabadiliko makubwa katika
uhifadhi, utumaji, upokeaji wa pesa na manunuzi ya kila siku katika
maeneo mbalimbali hapa nchini na sasa huduma hiyo inazaidi ya wateja
milioni tatu nchini kote.
Kwa takribani
miaka minne sasa huduma ya M-pesa imekuwa njia mbadala katika huduma za
kifedha kwa wateja wa kampuni hiyo. Huku jitihada za kuboresha na
kuongeza matumizi ya huduma hiyo yakiongezeka siku hadi siku, Vodacom
imefanikiwa kutengeneza mtandao wa mawakala zaidi ya elfu ishirini na
tano na kurahisisha upatikanaji wa huduma hiyo kwa wateja wote nchini.
No comments:
Post a Comment