UCHAGUZI NETIBOLI KUFANYIKA AGOSTI 11 DAR ES SALAAM
Na Mwandishi WetuCHAMA cha Netiboli Mkoa wa Dar es Salaam (CHANEDA),kinatarajia kufanya uchaguzi wa viongozi wake Agosti 11, mwaka huu jijini.
Akizungumza na gazeti hili jijini jana, Ofisa Habari wa CHANEDA,Michael Maurus pichani kulia, alisema kuwa uchaguzi huo unafanyika, ikiwa ni baada ya viongozi waliopo madarakani kumaliza muda wao tangu mwaka jana.
Alisema kuwa kuchelewa kufanyika kwa uchaguzi huo kulitokanana vyama vya wilaya za Ilala, Kinondoni na Temeke kutofanya chaguzi zao ilikupata wapiga kura halali ambao ndio watakaochagua viongozi wa mkoa.
“Ili uchaguzi ufanyike, lazima kuwapo
na wapiga kura halali ambao ni viongozi wa klabu na vyama vya netiboli
vya wilaya, tuliagiza vyamavifanye chaguzi, lakini hadi sasa hakuna
mwitikio wowote, hivyo tumeonatuwatumie viongozi wa klabu kufanya
uchaguzi huo wa mkoa ili viongoziwatakaopatikana wapange taratibu za
kufuatilia kila chama cha wilaya kuona ninikinaendelea huko,” alisema
Maurus.
Juu ya uchaguzi huo wa CHANEDA,
Maurus alisema kuwamchakato wa uchukuaji fomu na kurudisha, unaanza
Jumatatu ya Julai 23 hadi Julai 30, mwaka huu wakati usaili itakuwa ni
Agosti 4, mwaka huu.
Maurus alisema kuwa fomu za kuwania uongozi huozinapatikana katika ofisi ya Ofisa Michezo Mkoa wa
Dar es Salaam.
Kwa sasa viongozi waliobaki
wanaokisimamia chama hicho niMwenyekiti Winfida Emmanuel, Katibu Mkuu
Joseph Ng’anza na Maurus akiwa kamaOfisa Habari na Katibu Msaidizi.
Wengine waliokuwa na nafasi
CHANEDA ambao hata hivyohawakuwa karibu na chama hicho kutokana na
sababu mbalimbali, ni Jackson Henzron(Mweka Hazina), Christina Kimamla,
Mussa Sambala, Khadija Ally na Moshi Mganga (wotewajumbe), huku Makamu
Mwenyekiti akiwa ni Pili Mogella ambaye hata hivyo alijiondoakutokana na
kutohudhuria vikao.
No comments:
Post a Comment