Thursday, July 26, 2012

ALICHOKIANDIKA JOSE CHAMELEONE KUHUSU ERICK SHIGONGO KUENDELEA KUISHIKILIA PASSPORT YAKE.

Jose Chameleone akiperform wakati wa Usiku wa Matumaini, tamasha lililoweka Historia ya burudani 2012 kwa kuandaliwa na Global Publishers wakishirikiana na wadau wengine.

Kama kumbukumbu zako zipo fresh, muda mfupi baada ya Jose Chameleone kumaliza show yake Uwanja wa taifa July 7 2012 na kufanya kama walivyokubaliana kwenye mkataba, siku mbili baadae stori gazetini ziliandikwa kwamba mwimbaji huyu staa wa Uganda ameshindwa kurudi kwao kutokana na Passport yake ya kusafiria kushikiliwa na Eric Shigongo C.E.O wa Global Publishers walioandaa show hiyo kutokana na kumdai pesa ambazo ilidaiwa alishawahi kulipwa kipindi cha nyuma kuja kufanya show Tanzania lakini hakutokea.

Pamoja na hati yake ya kusafiria kuzuiliwa na Erick Shigongo, aliweza kusafiri kurudi kwao… sasa baada ya kuwa kimya kidogo…… hiki ndicho alichoandika kwenye ukurasa wake wa facebook kuhusu hiyo ishu.

Kwa ufupi ni kwamba Jose Chameleone amemlalamikia Big Boss Erick Shigongo kuhusu kuendelea kuishikilia Passport yake wakati meneja wake Chemeleone hakuhusika kuchukua hizo dola za Kimarekani 3500 zinazodaiwa kupokelewa na Meneja wa Chameleone kwa ajili ya show iliyopangwa siku nyingi kidogo.

Chameleone amesema aliporudi Uganda alifanikiwa kumkamata na kumpeleka polisi George, mtu ambae ndio anadaiwa kuzichukua hizo pesa akijidai ni meneja wa Chameleone lakini baadae akaachiwa huru ambapo baada ya kuona hivyo ilibidi Chemeleone aende kwa balozi wa Tanzania Uganda ili kupata msaada lakini hakufanikiwa. 

Amesema wakati passport yake ilipozuiliwa na Erick Shigongo alikwenda kwenye ubalozi wa Uganda Tanzania na ndio uliomsaidia kumpa Document zilizomuwezesha kurudi nyumbani, kwa sasa amepata mialiko ya shows South Africa, England, Belgium, Norway, Sweeden, Canada n.k lakini hajui itakuaje na anahitaji ushauri kuhusu Erick Shigongo ambae ameshikilia Passport yake kwa zaidi ya mwezi mmoja.
.
.(kwa Hisani ya millardayo.com)

No comments:

Post a Comment