MWENGE YATWAA KOMBE LA POLISI JAMII WILAYA YA KIPOLISI KINONDONI
Mkuu
wa Polisi Wilaya ya Kinondoni,(SSP)Willbrod Mutafungwa akisom risala
mbele ya mgeni rasmi Naibu meya wa manispaa ya Kinondoni Songoro
Mnyonge, wakati wa kufunga michezo ya Polisi jamii katika wilaya ya
Kipolisi Kinondoni juzi. (Picha na Abdallah Khamis)
Na Abdallah Khamis
TIMU ya Polisi
Jamii Mwenge, juzi ilijinyakulia zawadi ya shilingi milioni moja,
kikombe pamoja na jezi seti moja baada ya kuibamiza timu ya Polisi jamii
ya Mwananyamala Kisiwani kwa bao 1-0, katika fainali ya Polisi Jamaii
wilaya ya Kipolisi Kinondoni mchezo uliofanyika katika uwanja wa Biafra.
Katika
michuano hiyo iliyoanza julai 9 mwaka huu,mshindi wa pili timu ya Polisi
jamii Mwananyamala kisiwani ilijinyakulia sh.500,000, jezi pamoja na
Kikombe huku timu ya Polisi jamii Kinondoni muslim ikijipatia zawadi ya
Sh.250,000 kwa kuwa washindi wa tatu
Akikabidhi
zawadi kwa washindi mgeni rasmi katika fainali hizo Naibu meya wa
manispaa ya Kinondoni Songoro Mnyonge, alisema watahakikisha michezo
hiyo inakuwa endelevu kwa manispaa kushirikiana na jeshi la polisi
pamoja na wadau wengine ili kuwafanya vijana waepukane na uhalifu
Mnyonge alisema malengo ya mashindano yamefikiwa kwa kiasi kikubwa kwa kuwa vijana wa kata zote katika wilaya ya kipolisi Kinondoni, walipatiwa elimu ya
kuachana na madawa ya kulevya namna ya kutoa taarifa za kuzuia uhalifu
pamoja na kuachana na dawa za kulevya katika siku zote za mashindano.
Kwa upande
wake mkuu wa polisi wilaya ya Kipolisi Kinondoni Willbrod Mutafungwa
alisema timu zilizoshiriki zilikuwqa 14 kutoka katika kata nane za
wilaya hiyo.
Mutafungwa
ambaye pia ndiye alikuwa mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya michezo
hiyo alisema kwa kuwa ni mar ya kwanza kwea michezo hiyo kusimamiwa na
wilaya yake Kipolisi watahakikisha mapungufu yaliyojitokeza hayajirudii
pindi watakapoandaa michezo hiyo kwa wakati mwingine.
No comments:
Post a Comment