ABIRIA WATUMIAO MELI WAKABIDHIWE TIKETI NA 'LIFE JACKET' KWA PAMOJA DIRISHANI?
KUTOKANA
na ajali za mara kwa mara za Meli na boti za kusafirishia abiria, sasa
kuna umuhimu wa kila abiria anayekata tiketi dirishani apewe tiketi
pamoja na kifaa cha kuokolea maisha, 'Life Jacket'? kwa pamoja ili
kupunguza longolongo za wenye vifaa hivyo kutoa visingizio pindi
zitokeapo ajali kuwa vifaa vilikuwapo bali abiria hawakuvitumia?
Labda
hii itasaidia kuokoa maisha ya watu wengi pindi zinapotokea ajali kama
hizi zilizokwishatokea na pia itasaidia kuwafanya wahusika kubeba abiria
idadi sawa kulingana na uwezo wa Meli na idadi ya vifaa vilivyopo, hii
mnaionaje wadau?
Tena
Abiri inabidi uwe mkali pale dirishani wakati ukipewa tiketi yako
usipopewa life jacket, unahoji ''Vipi mbona hamnipi na Life Jacket''?.
No comments:
Post a Comment