Thursday, July 19, 2012

China Kutoa Dola Bilioni 20 Kwa Afrika

Rais Hu Jintao, Uchina ameziahidi serikali za Afrika mkopo karibu dola za Marekani bilioni 20 kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo.Amesema kuwa mkopo huo utasaidia katika ujenzi wa miundo mbinu, kilimo na maendeleo ya biashara.

Rais Jintao aliyasema hayo wakati wa mkutano wa ushirikiano baina ya Uchina na viongozi wa Afrika mjini Beijing.Kuanzia barabara mpya za mjini Nairobi hadi wauza kuku katika soko la Zambia ni dhahiri kwamba Uchina imeweka nyayo zake katika kuinua uchumi wa Mataifa mengi barani Afrika.
Miundo mbinu ni mojawapo ya sehemu ambazo Uchina imewekeza vilivyo barani Afrika.Biashara kati ya Bara Afrika na Uchina imeongezeka kutoka dola bilioni 10 miaka kumi iliyopita na kufikia takriban dola bilioni mia moja na sitini hii leo.
 Nchi hiyo imetoa mikopo zaidi kuliko Benki ya Dunia

No comments:

Post a Comment