WANANCHI WAGOMEA MRADI WA BENKI YA DUNIA
MRADI wa ujenzi dampo la kisasa wenye thamani ya
shilingi bilioni 3 unofadhiliwa na benki ya dunia katika jiji la Arusha, upo
hatari kuyeyuka kufuatia wananchi wa kata ya Muriet manispaa ya Arusha
kugoma kupisha eneo la mradi huo licha ya kulipwa stahili zao .
Aidha mradi huo ambao ulikuwa uanze tangu april mwaka
jana umeshindwa kuendelea kutokana na mvutano mkali ulipo kati ya wananchi
zaidi ya 200 na manispaa ya jiji la Arusha ,ambapo wananchi hao wameilalamikia
manispaa hiyo kwa kushindwa kuwalipa fidia ya maeneo yao waliyoyaendeleza ,huku manispaa hiyo
ikidai imeshawalipa.
Akizungumzia swala hilo
, Mkurugenzi wa manispaa ya Arusha, Bw Estomih Changa’h alikiri wananchi hao
kuwa kikwazo cha kuanza kwa mradi huo huku akidai kuwa wafadhili wa mradi huo
ambao tayari walionyesha nia na kuja na kupima katika eneo hilo wameanza kukata tamaa.
Alifafanua kuwa , baada ya kufanya tathmini ya awali
mwaka jana walibaini kuwa wananchi 42 ndio waliopo ndani ya eneo
husika la mradi ,hivyo manispaa ya Arusha ilifanya tathimin na kukubali
kuwalipa kiasi cha shilingi milioni 252 kama fidia ya makazi yao.
‘’tulipofanya tathimini ya makazi yao
tulikubaliana kuwalipa wakazi hao 42,na kila mtu alipigwa picha akiwa amesimama
mbele ya eneo ama nyumba yake,sasa tunasikitika sana kuona wakiendelea kunga’ng’ania huku
kundi lingine la watu zaidi ya 200 wakiibuka kutaka nao walipwe fidia’’alisema
Bw Chang’ah
Alisisitiza kuwa,tayari manispaa imeshawalipa wananchi
33 kati ya 42 kwa kiwango tofauti na kubaki wananchi tisa tu ambao walikuja
kurubuniwa na kugomea malipo hayo.
Aliongeza kuwa, wananchi hao wamekuwa wakifika katika
ofisi ya manispaa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha kudai fidia zao ambapo
wamekuwa wakijaribu kuwaelewesha na uendesha vikao kadhaa, lakini wamekuwa
wagumu kuelewa .
Mwenyekiti wa kamati ya waathirika hao ,Jackson
Japhet alisema kuwa, wao wanachotaka ni kutaka kulipwa fidia stahili ya makazi
yao kwani wengi wa wananchi wamekuwa wakiishi hapo muda mrefu na wamekuwa
na makazi ya kudumu ,hivyo ni ngumu sana wao kuondoka katika eneo hilo.
Wakizungumza katika kikao cha hadhara katika eneo hilo la Muriet mwishoni
mwa wiki, wameazimia kwenda mahakamani kusimamisha uanzishaji wa mradi huo
hadi manispaa hiyo itakapofanya tathimini upya kwa kuwashirikisha
wananchi hao na kuwalipa fidia stahili bila kuwapunja.

No comments:
Post a Comment