
Mwanza
imejipatia tiketi ya kucheza fainali ya michuano ya Copa Coca-Cola 2012
baada ya leo asubuhi (Julai 13 mwaka huu) kuilaza Temeke mabao 3-1
katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam.
Hadi
dakika 90 za kawaida zinamalizika timu hizo zilikuwa zimefungana bao
1-1. Mwanza walitangulia kufunga dakika ya tatu kupitia kwa Jamal
Mtegeta kabla ya Temeke kusawazisha kwa penalti dakika ya 56 iliyowekwa
wavuni na Baraka Ntalukundo.
Mabao
mengine ya Mwanza yaliyoipatia tiketi ya kucheza fainali keshokutwa
(Jumapili) yalifunga katika dakika 30 za nyongeza. Mtegeta alitikisa
wazu dakika ya 94 kabla ya Dickson Ambundo kukwamisha la tatu dakika ya
108.
Nusu
fainali ya pili itachezwa leo jioni ikikutanisha timu za Morogoro
ambayo kwenye robo fainali iliibamiza Mara mabao 4-0 na Tanga iliyopata
ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Dodoma.
No comments:
Post a Comment