Askari wanaolinda katika benki ya Posta
tawi la Metropolitan Posta jijini Dar es salaam wakimdhibiti kibaka
aliyemkwapua mhindi mmoja ambaye jina lake halikupatikana mara moja
baada ya kukimbilia katika benki hiyo ili kujiokoa na kipigo kutoka kwa
wananchi wenye hasira kali.
Tukio hilo
ambalo limesababisha huduma zote kusimama katika benki hiyo huku kukiwa
na purukushani kubwa wakati kibaka huyo akijaribu kujiokoa asipate
kichapo cha mbwa mwizi
Kibaka huyo akipambana vikali na
walinzi wa benki hiyo wakati alipokuwa kikimbilia ndani ya benki hiyo
huku askari huyo akimzuia kama anavyoonekana katika picha.
Kibaka huyo akiwa amedhibitiwa kabisa kana anavyoonekana akiwa amelala chini ndani ya benki hiyo.
Wahindi hawa ndiyo wanaodaiwa kutaka kukwapuliwa na kibaka huyo hapa wakiondoka katika eneo la benki hiyo.






No comments:
Post a Comment