Friday, July 13, 2012

WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII YAKUTANA NA UJUMBE WA BIASHARA NA UWEKEZAJI WA HUDUMA ZA AFYA KUTOKA NCHINI NETHERLAND

Kaimu mgaga mkuu wa serikali Dkt. Donan Mmbando akizungumza na ujumbe wa Biashara na Uwekezaji katika huduma za afya kutoka nchini Netherland  mara baada ya ujumbe huo kuwasili makao makuu ya Wizara ya Afya na Ustawi  wa jamii jana jijini Dar es Salaam.

Kamishina wa Idara ya Ustawi wa Jamii wa Wizara ya Afya  Bw. Danford Makala (kulia) akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali kuhusu Ustawi wa jamii wakati wa mkutano  kati ya Ujumbe  wa Biashara na Uwekezaji katika huduma za afya kutoka nchini Netherland na watendaji wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii jana jijini Dar es salaam.
 
Meneja Mkuu na mmiliki wa Hospitali zinazojengwa kwa kutumia makontena (Hospitainer) na kuweza kupelekwa kutoa huduma  za afya maeneo yoyote  kutoka nchini Netherland Bw. Rolof Mulder akiongea na watendaji wa wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kuelezea namna kampuni hiyo inavyofanya kazi zake.
 
Baadhi ya viongozi wa ujumbe wa Biashara na Uwekezaji katika huduma za afya kutoka nchini Netherland  wakifuatilia fafanuzi mbalimbali zilizokuwa zikitolewa na watendaji wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii jana jijini Dar es salaam.
 
Watendaji wakuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii wakiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa Biashara na Uwekezaji katika huduma za afya kutoka nchini Netherland .

No comments:

Post a Comment