OKWI BADO ANA MKATABA SIMBA
Makamu mwenyekiti wa SIMBA KABURU akionyesha mkataba wa OKWI ambaye bado
ana mkataba wa kuichezea timu hiyo .Simba umesikitishwa na habari
zilizovumishwa kwenye vyombo vya habari kuhusu mshambuliaji huyo wa
kimataifa wa Uganda kujiunga na wapinzani wa jadi, Yanga SC.
Akizungumza na Waandishi wa Habari mchana wa leo, makamu Mwenyekiti wa
Simba, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’, alisema kwamba habari hizo hazina
ukweli wowote, ni kinyume cha maadili ya taaluma ya uandishi wa habari
na zina lengo la kupotosha ukweli na kuwanyima raha wale wote wenye
mapenzi mema na Simba.
No comments:
Post a Comment