NSSF YAPATA TUZO MBILI KATIKA MAONYESHO YA SABASABA
Makamu
wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya zanzibar, Balozi Seif Ali
Idi akito hotuba yake katika ufunguzi wa Maonyesho ya Biashara ya
Kimataifa Barabra ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Pili wa Rais wa Seriakli ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), Balozi Seif Ali Idi akifungua rasmi Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa maarufu kama sabasaba.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Seriakli ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), Balozi Seif
Ali Idi akimkabidhi cheti pamoja na tuzo Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la
Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dk Ramadhan Dau baada ya kuibuka
washindi wa jumla katika Maonyesho ya 36 ya Biashara ya Kimataifa Jijini
Dar es Salaam.
Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka wa TANTRADE, Samuel Mvingira akizungumza
wakati wa ufunguzi wa Maonyesho ya 36 ya Biashara ya Kimataifa katika
viwanja vya Mwalimu Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Viwanda Biashara na Masoko, Dk Abdallah Kigoda akizungumza katika hafla hiyo.
Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dk Ramadhan Dau
akiongea na Waandishi wa Habari muda mfupi baada ya kukabidhiwa tuzo na
cheti cha Ushindi wa Jumla katika maonyesho ya 30 ya Biashara ya
Kimataifa (Sabasaba) Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dk Ramadhan Dau
akiwa pamoja na Maafisa wengine wa NSSF wakifuatilia Hotuba ya Ufunguzi
wa Maonyesho hayo.
Maafisa wa NSSF wakifuatilia hotuba ya mgeni Rasmi.
Maafisa wa NSSF wakiwa kwenye Banda lao.
Huduma zikiendelea kutolewa.
No comments:
Post a Comment