Baadhi ya wachezaji wa Bongo Fleva wakiwa mazoezini.
Bongo Fleva wakiwa ‘siriaz’ mazoezini.
Kala Pina (katikati), akipasha misuli na wenzake.
Mchezaji wa Bongo Fleva, Suma G akijinoa.
Vicent Kigosi ‘Ray’ wa Bongo Movie akijiwinda kwa mpambano wa Jumamosi.
Inspector Haroon wa Bongo Fleva akiwa mazoezini.
---
TIMU
za mpira wa miguu za wasanii wa muziki, Bongo Fleva, na wacheza sinema,
Bongo Movie, jana zilizidi kutoleana vitisho kwenye mazoezi
yaliyozikutanisha katika Viwanja vya Leaders Club Kinondoni jijini Dar
es Salaam.
Mwenyekiti wa Timu ya Bongo
Movie, Jacob Steven ‘JB’, alisikika akisema kuwa hakuna mechi itakuwa
chungu kwa Bongo Fleva kama ya Tamasha la Matumaini itakayofanyika
Jumamosi hii, ambapo wanatarajia kuwapakiza mvua ya magoli.
Nao Bongo Fleva, kupitia mchezaji
wao Kala Pina, walisema mazoezi wanayoyapata kutoka kwa kocha wao,
Seleman Matola, wanawaomba Bongo Movie wajitoe mapema mechi hiyo kwani
moto wake utakuwa mkali isivyo kawaida.
No comments:
Post a Comment