Meneja wa bia ya Serengeti Lager Bw. Allan Chonjo akikabidhi kadi ya
usajili wa Bajaj aliyojishindia Bw Richard Mbezi wa jijini baada ya
kushinda katika bahati nasibu ya Promosheni ya Vumbua Dhahabu Chini ya
Kizibo inayoendesha na kampuni ya bia ya Serengeti kupitia bia zake za
Serengeti. Tusker na Pilsner, mkabidhiano hayo yalifanyika jana katika
bonanza la Serengeti Fiesta Soccer Bonanza katika viwanja vya TCC Sigara
Chang'ombe jijini Dar es salaam.
Bw. Mbaraka Adam mshindi wa Pikipiki katika promosheni ya Vumbua
Dhahabu chin i ya Kizibo akipanda pikipiki yake mara baada ya
kukabidhiwa kwenye viwanja vya TCC Sigara Chang'ombe jijini Dar es
salaam, kulia katika picha ni Allan Chonjo Meneja wa bia ya Serengeti,
Bahati Singh Meneja wa Matukio na Promosheni.
Meneja Matukio na Promosheni wa kampuni ya bia ya Serengeti Bahati Singh
akimuelekeza kitu Bw. Richard Mbezi mara baada ya kukabidhiwa jana
kwenye viwanja vya TCC Sigara jana, kushoto ni Allan Chonjo Meneja wa
bia ya Serengeti.



No comments:
Post a Comment