TAARIFA KWA WANANCHI JUU YA ZOEZI LA SENSA YA TAIFA-2012
Watanzania
wenzangu kama tunavyofahamu mwaka 2012 ni mwaka ambao nchi yetu
inafanya zoezi maalumu la sensa ya taifa. Sensa hii inafanyika kila
baada ya miaka kumi, sensa ni zoezi maalumu linalofanya na serikali ili
kuesabu watu na makazi, na lengo lake ni takwimu sahii zitazopatikana
katika zeozi hili zitumike katika taratibu maalumu za mikakati ya
serikali kupanga utaratibu wa maendeleo kwa wananchi wa nchi yake.
Mfano, mimi ni miongoni mwa watanzania waliobahatika kuhusika katika
sensa ya marakani iliyofanyika miaka michache iliyopita chini ya idara
ya takwimu, wizara ya kazi na ilikuwa elimu ya mafunzo kama mwanafunzi (
internship). Kwahiyo si vibaya kutumia muda huu ili kueleza kile kidogo
nilichoweza kujifunza katika zoezi hili watanzania wenzengu waweze
kufaidika na umuhimu wa zoezi hili.
Utangulizi
Zoezi la
sensa ya taifa litafanyika mwezi wa August 25 kuamkia 26 mwaka huu 2012.
Zoezi hili linasimamiwa na Idara ya ofisi ya Takwimu, chini ya wizara
ya fedha. Idara hii inaongozwa na Dk. Albima Chuwa. Tanzania chini ya
idara hii ya takwimu inatumia technologia ya kisasa iitwayo Optcal Mark
reader kwa maarufu ni ufundi wa scanning wa kitechnologia ambao ni nchi
chache katika bara la Afrika wanazotumia. Zoezi hili la sensa
lilifanyika mwaka 2002 na liliweza kufanikiwa kwa kiwango cha juu na
kuzifanya baadhi ya nchi nyingi barani la Afrika kuja nchini Tanzania
kujifunza katika miaka hii michache juu ya mafanikio yaliyopatikana na
idara hiyo ya takwimu ya serikali. Mfano wa nchi ambazo wameweza
kujifunza na kufuata taratibu hizi kwenye idara ya takwimu ni Ghana,
Angola, Sudan,Ethiopia, Elitrea na Lesotho. Si hivyo tu, kutokana na
Tanzania kuwa na mfumo ambao ni imara na wakuweza kutoa taarifa za
takwimu sahii za zoezi hili ukilinganisha na nchi nyingine katika bara
la Afrika, Tanzania imeweza kuwa mjumbe wa kamisheni ya takwimu ya umoja
wa mataifa kwa muda wa miaka minne kuanzia january 2012 na sababu kubwa
iliyotokana na umairi na ukufuzi, usimamizi na mafunzo yanoyotolewa
katika ngazi ya taifa, mkoa, wilaya, kata na makarani wa zoezi hilo na
kufanikisha kutoa takwimu sahii ukilinganishwa na nchi nyingine barani
afrika. Kama tunavyofahamu sensa hufanyika na mataifa mbali mbali
duniani. Tanzania inafuata mfumo wa kufuata kanuni, taratibu na miongozi
uliwowekwa na umoja wa mataifa.
Nini maana ya sensa ?
Sensa ya
watu na makazi ni utaratibu wa serikali wa kukusanya, kuchambua ,
kutathmini na kuchapisha au kusambaza takwimu za kidemografia ,kuichumi
na kijamii kuhusiana na watu wote na makazi yao katika nchi kwa kipindi
maalumu ( kawaida ni miaka kumi). Kwa maana nyingine ni zoezi maalumu
linafanywa na serikali lenye utaratibu ambao unakusanya taarifa za idadi
ya watu na makazi na kuzitumia takwimu hizo za taarifa kuweza
kutathimini ubora wa hali ya maisha ya watanzanzia na kuiwezesha
serikali kupanga na kutekeleza mipango ya maendeleo kwa lengo la
kuboresha maisha ya wananchi wake.
Nini lengo la sensa?
Lengo
la zoezi la sensa litaiwezesha serikali kuwa na takwimu sahii kuhusiana
na watu ambazo zitachangunua na kuainisha kwa makundi, ukubwa,
mtawanyiko au msongamano wa watu na makazi katika maeneo yote ya nchi.
Vile vile, taarifa za sensa zinaweza kuisaidia serikali katika kupanga
na kutekeleza mipango yake ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii. Mfano,
takwimu hizi zinazotokana na zoezi la sensa zinaisaidia serikali kujua
mahitaji halisi ya wananchi wa Tanzania yakiwemo makundi yenye mahitaji
maalumu, mathali ya watu wenye ulemavu, na kuiwezesha serikali kuwa na
mipango ya maendeleo ya muda mfupi na mrefu. Kwahiyo madhumuni makuu ya
sensa ya taifa ni kujua idadi ya watu na makazi nchini pamoja na
kukusanya taarifa zao muhimu kama vile umri, jinsia, mahali wanapoishi,
hali ya ndoa, kiwango cha elimu, hali ya ajira, hali ya uzazi na vifo,
hali ya makazi na taarifa nyinginge muhimu kwa maisha yao ya kila siku.
Si, mara ya
kwanza Tanzania kufanya zoezi hili la sensa, sensa iliweza kufanyika
katika miaka ya 1967, 1978,1988, na 2002. Kama nilivyotangulia kusema
mwaka huu 2012 sensa itafanyika August 26. La kutia moyo miaka hii ya
karibuni limeweza kufanyika kwa ufanii zaidi. Na ndiyo maana ripoti za
kimataifa zinaonyesha Tanzania katika kipindi cha miaka kumi kumeweza
kupiga hatua katika nyanja mbali mbali za kiuchumi na kijamii. Mfano,
kutokana na taarifa ya benki ya dunia inoenyesha Tanzania ni miongoni
mwa nchi ambazo zimeweza kufanikiwa kuwa na mikati imara ya elimu kwa
wananchi wake, huduma ya afya na sekta mbali mbali za uchumi kama vile
kilimo na kuifanya nchi kukuza uchumi wake kwa asilimia 6.7 kwa mwaka
ikilinganishwa na nchi nyingine duniani kama vile china na india,
kutokana na taarifa sahii za takwimu zilizoweza kupatika katika sensa ya
2002.
Kama
tunavyofahamu malengo makubwa ya mikakati ya kuuza uchumi na kupunguza
umaskini (MKUKUTA) kwa upande wa Tanzania bara ni kukuza uchumi na
kupunguza umaskini wa kipato, kuinua kiwango cha maisha na ustawi wa
jamii na kuimarisha utawala bora na uwajibikaji. Na kwa upande wa
Zanzibar mpango huu unajulikana kama MKUZA wenye malengo matatu:
1. Ukuzaji wa uchumi
2. Ustawi wa jamii ulio bora
3. Ujenzi wa misingi ya utawala bora
Hivyo
basi tunaimani kabisa taasi husika litalifanya zoezi hili kufanyika kwa
ufanisi zaidi kama lilivyoweza kufanyanyika mwaka 2002. Kutokana na
Uzoefu wangu wa Intership ya zoezi hili nilioupata hapa marekani,
tungeweza kuishauri mamlaka husika kuendelea kutoa mafunzo maalumu
katika ngazi zote za taifa, mikoa, wilaya, kata na makarani. Kuweza
kuakikisha vifaa muhumu vya kitechnolojia vinasambazwa kwa muda muafaka
bila kuchelewa. Vile vile, wahusika wakubwa katika kutoa taarifa kama
vile walimu, wenyeviti wa vijiji na wahusika wakuu kutoa taarifa zilizo
sahii.
Wito kwa wahusika kufanikisha zoezi hili
Kwahiyo
tunatoa wito kwa vyombo vyote vya habari magazeti mbalimbali, redio,
vituo vya televisions,blogs na websites mbali mbali watumie fursa hii
kuwaelimisha watanzania ni nini maana ya sensa na malengo yake. Wito
kwa wadua mbali mbali kama vile, viongozi wa wa umini wa dini ya
kikristo, kiislamu na watu wa madhehebu mbalimbali kutumi kipindi hiki
kifupi kuelewesha watanzania umuhimu wa zoezi hili. Kwa wale wadau wa
vyuo na wanasanaa watumie fursa hii kwa kutumia ngojera, kwaya ,
mashairi na ngoma na utamaduni wa mtanzania kwa lengo la kuilewesha umma
juu ya umuhimu wa zoezi hili. Tunamatumaini makubwa wa wahusika wa
maeneo muhimu wa utoaji habari muhimu katika sensa kama vile hospitali,
vyuo, shule , kambi za jeshi, kambi za wakimbizi, nyumba za kulala
wageni na magereza mmejipanga vizuri katika zoezi hili. Nimatumaini
yangu zoezi la sensa ya Taifa la mwaka 2012 litafanyika kwa ufanisi
zaidi bila wasiwasi ili taarifa mbali mbali kama vile shule,, vyuo,
hospitali, vituo vya afya, zahanati, masoko, huduma za fedha, majosho,
vyanzo vya maji, miundo mbinu kama vile barabara, madaraja na
mawasiliano zitazopatikana zitakuwa sahii. Hivyo taarifaa
itakayopatikana katika zoezi hili la sensa litaweza kuisaidia serikali
kutimiza malengo yake ya kupanga mikakati ya maendeleo kwa watanzania
kama vile mikakati ya kukuza uchumi na kupunguza umaskini kwa kupunguza
umaskini wa kipato, kuinua kiwango cha maisha na ustawi wa jamii kwa
kuboresha humuma muhimu za watanzania kama vile elimu, na afya. Na
mpango, kutimiza mpango muhimu wa serikali wa 2015 wa mpango wa
maendeleo ujulikanao Milenium.
Mwisho,
tunawatakia watendaji wote wa serikali mafanikio mema ya utendaji
katika zoezi hili muhimu la serikali kuanzia idara ya takwimu za taifa,
mikoa, wilaya, tawi na watendaji. Rekodi inaonyesha zoezi hili
lilipofanyika mwaka 2002 lilifanyika kwa ufanisi wa viwango vilivyowekwa
na umoja wa mataifa na kuweza kuitangaza Tanzania kuwa mwalimu wa
mafunza wa nchi nyingine barani afrika kama vile Ghana, Angola, Sudan,
Ethiopia, Elitrea na lesotho.
Kwaniaba
ya watanzania waishio nje ya nje, tunatoa pongezi kwa kulitumikia taifa
letu changa na lenye bajeti ndogo na mazingira magumu ya kazi. May god
bless you
Mungu ibariki Tanzania
Asanteni
Katibu wa Tawi CCM Washington DC
Yacob Kinyemi
No comments:
Post a Comment