MATUKIO MBALIMBALI YA ZIARA YA RAIS KIKWETE NCHINI UINGEREZA
Rais
Jakaya Mrisho kikwete, Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda na mkewe
Mama Janet Museveni, Waziri Mdogo wa Uingereza wa Maendeleo ya Kimataifa
Bw. Stephen O'Brien (kulia) na Mama Melinda Gates wakibadilishana
mawazo kabla ya kuhutubia katika mkutano wa kimataifa wa viongozi
kujadili Uzazi wa Mpango kwa nchi masikini zaidi duniani katika ukumbi
wa Queen Elizabeth II jijini London July 11, 2012. Mkutano huo ni wa
kwanza wa aina yake duniani na umeanzisha Mchakato wa Dunia ambao
utalenga kuwawezesha wanawake wapatao milioni 120 katika nchi masikini
zaidi duniani kupata habari, huduma na mahitaji ya kupanga uzazi bora
zaidi na kuokoa maisha yao ifikapo mwaka 2020.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akuhutubia katika mkutano wa kimataifa wa
viongozi kujadili Uzazi wa Mpango kwa nchi masikini zaidi duniani,
katika ukumbi wa Queen Elizabeth II jijini London July 11, 2012. Mkutano
huo ni wa kwanza wa aina yake duniani na umeanzisha Mchakato wa Dunia
ambao utalenga kuwawezesha wanawake wapatao milioni 120 katika nchi
masikini zaidi duniani kupata habari, huduma na mahitaji ya kupanga
uzazi bora zaidi na kuokoa maisha yao ifikapo mwaka 2020.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Waziri Mkuu wa Uingereza Bw. Donald
Cameron, Rais Paul Kagame wa Rwanda na Rais Yoweri Kaguta Museveni wa
Uganda wakijiandaa kupanda jukwaani kuhutubia katika mkutano wa
kimataifa wa viongozi kujadili Uzazi wa Mpango kwa nchi masikini zaidi
duniani. katika ukumbi wa Queen Elizabeth II jijini London July 11,
2012. Mkutano huo ni wa kwanza wa aina yake duniani na umeanzisha
Mchakato wa Dunia ambao utalenga kuwawezesha wanawake wapatao milioni
120 katika nchi masikini zaidi duniani kupata habari, huduma na mahitaji
ya kupanga uzazi bora zaidi na kuokoa maisha yao ifikapo mwaka 2020.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake katika mazungumzo na Afisa
Mtendaji Mkuu wa British Gas (BG Group), Sir Frank Chapman (wa pili
kulia) na maafisa waandamizi wa kampuni hiyo. BG Group imewekeza kiasi
cha Pauni 80 za Uingereza (Shilingi Trilioni 125) katika mradi wa
kuchimba gesi asilia nchini Tanzania, na tayari visima vitano vya
nishati hiyo vimeshatema gesi nyingi katika bahari kuu kusini mwa
Tanzania maeneo ya Mtwara. Hii ilikuwa ni ziara fupi katika makao makuu
ya BG Group mjini Reading, Uingereza ambako Rais Kikwete na ujumbe wake
walitembelea Julai 11 kujionea namna kazi za uvumbuzi wa gesi asilia
unavyofanywa na kampuni hiyo yenye kufanya shughuli zake katika nchi 21
katika mabara matano, ikiwa na jumla ya wafanyakazi 6,000.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Afisa Mtendaji Mkuu wa British Gas
(BG Group), Sir Frank Chapman alipotembelea makao makuu ya kampuni hiyo
mjini Reading Uingereza Julai 11, 2012. BG Group imewekeza kiasi cha
Pauni 80 za Uingereza (Shilingi Trilioni 125) katika mradi wa kuchimba
gesi asilia nchini Tanzania, na tayari visima vitano vya nishati hiyo
vimeshatema gesi nyingi katika bahari kuu kusini mwa Tanzania maeneo ya
Mtwara. Hii ilikuwa ni ziara fupi katika makao makuu ya BG Group mjini
Reading, Uingereza ambako Rais Kikwete na ujumbe wake walitembelea Julai
11 kujionea namna kazi za uvumbuzi wa gesi asilia unavyofanywa na
kampuni hiyo yenye kufanya shughuli zake katika nchi 21 katika mabara
matano, ikiwa na jumla ya wafanyakazi 6,000.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wakipata maelezo ya maendeleo ya
uchimbaji wa gesi asilia nchini Tanzania walipotembelea makao makuu ya
British Gas (BG Group), ambayo imewekeza kiasi cha Pauni 80 za
Uingereza (Shilingi Trilioni 125) katika mradi wa kuchimba gesi asilia
nchini Tanzania, na tayari visima vitano vya nishati hiyo vimeshatema
gesi nyingi katika bahari kuu kusini mwa Tanzania maeneo ya Mkoa wa
Pwani na Mtwara. Hii ilikuwa ni ziara fupi katika makao makuu ya BG
Group mjini Reading, Uingereza, ambako Rais Kikwete na ujumbe wake
walitembelea Julai 11 kujionea namna kazi za uvumbuzi wa gesi asilia
unavyofanywa na kampuni hiyo yenye kufanya shughuli zake katika nchi 21
katika mabara matano, ikiwa na jumla ya wafanyakazi 6,000.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri Mdogo
wa Maendeleo ya Kimataifa wa Uingereza Bw. Stephen O'Brien jijini
London, ambapo Uingereza iliahidi kuendelea kuisaidia Tanzania katika
mambo mbalimbali ya maendeleo ikiwa ni pamoja na kusaidia kuendeleza
sekta ya nishati hususan utafutaji wa gesi asilia.
Waziri
wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt Hussein Mwinyi akiongea na baadhi ya
wajumbe wa mkutano wa kimataifa wa Uzazi wa Mpango katika ukumbi wa
Queen Elizabeth II jijini London Julai 11, 2012. Kushoto ni Mkurugenzi
Mtendaji wa Chama cha Uzazi na Malezi Bora Tanzania (UMATI), Bi
Josephine Mwankusye na kulia ni Naibu Mkurugenzi wa Afya ya Mzazi na
Mtoto katika Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt Neema
Rusibamayila.PICHA NA IKULU.
No comments:
Post a Comment