KUONDOKA KWA KALALA JR BENDI YA MAPACHA 3 HAITAYUMBA
Pichani
kati ni Mwanamuziki mahiri Josee Mara akifafanua kuhusiana na mikakati
yao waliyonayo kwa sasa mara baada ya mwanamuziki mwenzao mmoja,Kalala
Jr kutimka na kuwaacha wakiwa wawili badala ya watatu.Josee Mara amesema
wao wako fiti na hakuna kilichoharibika,kwani kuna wanamuziki wengine
kadhaa ambao ni wazuri na watafanya nao kazi kama ilivyokuwa kwa Kalala
Jr."Na sasa hivi nakuhakikishia Da'Suzzy tutapiga kazi ile mbaya,kwa
sababu hao vijana tunaowaongeza ni wanamuziki wazuri na tunawahamu toka
kitambo,kwa hivyo naamini mambo yatakuwa sawa na washabiki wetu
wasivunjike moyo,waendelee kutuunga mkono tu,sisi ni wapambanaji kwa
hiyo ni lazima tupambane"amesema Josee Mara.Aidha Khalid Chokoraa
ameongeza kuwa katika kuonesha bado wako fiti wamekwisharekodi singo
yao moja iitwayo ONA NAONEWA,ambayo wataitambulisha hivi karibuni kwa
mashabiki wa muziki wa dansi
Mmoja
wa watangazaji wa Clouds FM,kupitia kipindi cha Wikend Bonanza,Da'
Suzzy akizungumza na wanamuziki mahiri wa dansi hapa nchini waliokuwa
wakijiita Mapacha 3,ambapo kwa sasa mmoja wao Kalala Jr ameamua kuachia
ngazi na kuwaacaha wenzake Khalid Chokoraa na Josee Mara kama uwaonavyo
pichani wakiwa na Meneja wao Hamis Dacota pichani kulia.Da'Suzzy alikuwa
akitaka kujua kwanini msanii mwenzao Kalala Jr ameamua kutimka kwenye
bendi yao na kwamba wana mikakati gani ya kuliziba pengo la mwanamuziki
huyo aliyetimka.Kwa mujibu wa Meneja wa bendi hiyo ya Mapacha 3,Hamis
Dacota amebainisha kuwa Kalala Jr aliamua kuondoka mwenyewe bila kuwepo
na ugomvi wowote baina yao,"hivyo kama mwanamuziki mwenzetu,kijana
mwenzetu tunamtakia kila kheri huko aendako,lakini kama akitaka kurudi
pia milango iko wazi anakaribishwa sana,kwa sababu yeye ni mmoja wa
waasisi wa bendi ya mapacha 3",alisema Dacota
No comments:
Post a Comment