FIFA NA CAF KUFANYA MKUTANO NA WAANDISHI WA HABARI LEO
Mjumbe
wa Kamati ya Tiba ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) na
Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), Dk. James Sekajugo
atakuwa na mkutano na waandishi wa habari leo mchana.
Mkutano huo utafanyika saa 8 mchana kwenye ukumbi wa mikutano wa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Dk.
Sekajugo kutoka Uganda yuko nchini kusimamia upimaji umri (MRI Test)
kwa wachezaji wa timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17
(Serengeti Boys) uliofanyika jana kwenye hospitali ya Aga Khan, Dar es
Salaam.
Upimaji
huo umefanyika kutokana na maagizo ya CAF kuwa wachezaji wote
wanaoshiriki michuano ya Afrika kwa umri chini ya miaka 17 ni lazima
wapimwe kipimo cha MRI Test ndipo waruhusiwe kucheza.
Serengeti Boys imepangiwa kucheza Septemba mwaka huu dhidi ya Kenya katika raundi ya kwanza ya michuano hiyo.

No comments:
Post a Comment