Mabingwa
watetezi wa Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kombe la Kagame) Dar
Young African, wataanza kutetea ubingwa wao Julai 14 mwaka huu dhidi ya
Atletico ya Burundi mchezo utakaochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, leo Katibu Mkuu wa Baraza
la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), Nicholas
Musonye, ametangaza ratiba ya michuano hiyo wakati wa mkutano na
waandishi wa habari uliofanyika katika ofisi za Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF).
Musonye,
alisema kuwa jumla ya timu 11 zimethibitisha kushiriki katika michuano
hiyo itakayoanza Julai 14 hadi 28 mwaka huu, ambapo kwa siku zitachezwa
mechi mbili (saa 8 mchana na saa 10 jioni) huku Tanzania Bara
ikiwakilishwa na Yanga, Simba na Azam.
Mechi
ya kwanza siku ya ufunguzi kati ya APR ya Rwanda na Wau Salaam ya Sudan
itaanza saa 8 mchana, wakati Mabingwa watetezi wa Kombe hilo, Yanga ya
Dar es Salaam, watashuka dimbani saa 10, jioni kuvaana na Atletico ya
Burundi.
Aidha
Musonye aliyataja makundi kuwa ni Kundi A lina timu za Simba, URA ya
Uganda, Vita Club ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) na Ports ya
Djibouti.
Wakati timu za Azam, Mafunzo ya Zanzibar na Tusker ya Kenya zipo katika kundi B.
Yanga inaunda kundi C lenye timu za APR ya Rwanda, Wau Salaam ya Sudan Kusini na Atletico ya Burundi.
Aidha
Musonye, alisema kuwa katika michuano hiyo, jumla ya timu nane
zitaingia hatua ya robo fainali itakayochezwa Julai 23 na 24 mwaka huu.
Na
kundi A na C kila moja litatoa timu tatu kwenda robo fainali wakati B
litatoa timu mbili.El Merreikh ya Sudan, Red Sea ya Eritrea, Coffee ya
Ethiopia na Elman ya Somalia hazitashiriki katika mashindano ya mwaka
huu ambayo yanafanyika Tanzania Bara kwa mwaka wa tatu mfululizo
kutokana na sababu mbalimbali.
Coffee
haitashiriki kwa vile ligi ya Ethiopia inaanza Julai 14 mwaka huu
wakati El Merreikh wikiend ya Julai 13-15 mwaka huu itakuwa na mechi ya
michuano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).
Musonye,
alitaja zawadi ya Bingwa wa michuano hiyo ya mwaka huu kuwa
atajinyakulia kitita cha dola za Marekani 30,000/= na msindi wa pili
ataibuka na dola 20,000/= na mshindi wa tatu dola 10,000.
Michuano hiyo itakuwa ikionyeshwa moja kwa moja (live) na Televisheni ya SuperSport
No comments:
Post a Comment