Uokoaji umetarajiwa kuanza tena
leo huko mashariki mwa Uganda ambako vijiji vitatu vilifunikwa na
udongo kutokana na maporomoko ya udongo.
Shirika la msalaba mwekundu Uganda limesema zaidi ya watu 18 wamefariki dunia katika maporomoko hayo.
BBC wameandika kwamba zaidi ya nyumba kumi na tano zimefunikwa kutokana na mvua kubwa.
Hata hivyo bado waliojeruhiwa
kwenye eneo hilo wanaendelea kutibiwa baada ya kilichotokea kwenye eneo
hilo lenye rutuba la Bududa, linalokuza kahawa na lililopo karibu na
mbuga ya wanyama ya mlima Elgon.
No comments:
Post a Comment