Kama ulidhani maafa kama haya
ya maafuriko yanaweza kuchukua maisha ya watu kwenye nchi masikini peke
yake utakua umekosea, hata Uingereza kwa Malkia hichi kitu kimetokea leo
sema tu kuna utofauti mkubwa wa mazingira ya matukio.. wenzetu mvua
imenyesha kubwa lakini miundombinu yao inaruhusu kuyasafirisha maji kwa
hiyo hata kama yakisimama sio mengi sana.
Gazeti la The sun
limethibitisha kwamba mwanaume mmoja anaekadiriwa kuwa na umri wa miaka
90 ambae bado hajatambulika alizombwa na maji ya mvua kubwa iliyonyesha
saa nne asubuhi june 28 2012 ambapo mashahidi wamesema mwili wake
ulipatikana baada ya msako uliowahusisha police, zima moto na waokoaji
wengine ambapo alikutwa kwenye gari lake akiwa amefunikwa na maji.
No comments:
Post a Comment