Monday, June 25, 2012

TAMASHA LA WAZI LA AIRTEL JIUNGE NA SUPA5 LAITIKISA JIJI LA MWANZA

 Meneja Mahusiano wa kampuni ya simu za mikononi ya Airtel-Tanzania,Jackson Mmbando akimkabidhi Jamila Juma simu ya mkononi aina ya Sumsung,baada kuibuka mshindi kwa kuichammbua vyema huduma mpya ya Airtel Jiunge na Supa5.
 
 Pichani shoto wakazi wa Mwanza, Jamila Juma na  Sandra Mwashitete wakipewa maelekezo mafupi namna ya kutumia mtandao wa Airtel pamoja na huduma zake mbalimbali, mara baada ya kujishindia simu aina ya Sumsung,wakati kampuni ya Airtel ilipokuwa ikizindua huduma yake mpya ya Airtel Jiunge na Supa5,uliofanyika jana kwenye viwanja vya Furahisha,jijini Mwanza.
 
 Ni Mzee wa Makamo hivi lakini alionesha umahiri wake mkubwa wa kuwachangamsha vilivyo sehemu ya wakazi wa jiji la Mwanza.Anaitwa Mzee Salum akikamua jukwaani jana kwenye viwanja vya Furahisha jijini Mwanza,wakati wa uzinduzi  wa huduma mpya ya Airtel Jiunge na Supa5.
 
 Sehemu ya wakazi wa jiji la Mwanza waliojitokeza kwa wingi jana jioni kwenye uzinduzi ramsi wa huduma mpya ya Airtel Jiunge na Supa5,uliofanyika kwenye viwanja vya Furahisha jijini humo.
 
 Msanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya na kiongozi wa kundi la Wanaume Halisi kutoka Temeke,jijini Dar,akiwa sambamba na msanii mwenzake (hayupo pichani) aitwaye Kr-Mulla wakilishambulia jukwa huku shangwe kubwa ikilipuka kutoka kwa sehemu kubwa ya wakazi wa jiji la Mwanza waliojitokeza jana wakati wa uzinduzi rasmi wa huduma mpya ya Airtel Jiunge na Supa5.
 
 Baadhi ya wasanii wa kikundi cha Kinonko chenye maskani yake pale Kinondoni,kikionesha umahiri wake wa kucheza mbele ya umati mkubwa wa wakazi wa jiji la Mwanza waliojitokeza kwenye viwanja vya Furahisha wakati wa uzinduzi rasmi wa huduma mpya ya Airtel Jiunge na Supa5.
 
.Baadhi ya Wakazi wa jiji la Mwanza wakiendelea kuhamia Airtel na kupata huduma mbalimbali za kampuni hiyo,jana jioni kwenye  viwanja vya Furahisha wakati wa uzinduzi rasmi wa huduma mpya ya Airtel Jiunge na Supa5.

No comments:

Post a Comment