Monday, June 25, 2012

TUZO YA DHAHABU YA NDOVU

 Mpishi Mkuu wa Kampuni ya bia Tanzania TBL Gaudence Mkolwa, akipokea tuzo ya kimataifa ijulikanayo kama “Grand Gold Award”kutoka kwa Meneja wa bia ya Ndovu Special Mult Pamela Kikuli, baada ya kukabidhiwa na Meneja wa Wateja wa kampuni ya kimataifa ya kusafirisha mizigo DHL Busegi Kulwa (kulia), jijini Dar es Salaam kushoto ni Meneja wa habari na mawasiliano Edith Mushi.
 Grand Gold Award
Meneja wa Wateja wa kampuni ya kimataifa ya kusafirisha mizigo DHL Busegi Kulwa, akikabidhi tuzo ya dhahabu yenye hadhi ya juu zaidi ya ubora wa bidhaa kimataifa ijulikanayo kama “Grand Gold Award” kwa Meneja wa bia ya Ndovu Special Mult Pamela Kikuli, baada ya kinywaji hicho kinachozalishwa na kampuni ya bia Tanzania TBL, kupata tuzo hiyo kwa mara ya pili mfululizo.


MENEJA wa wateja wa kampuni ya kimataifa ya kusafirisha mizigo DHL Busegi Kulwa, amesema kampuni yao inajiskia faraja sana kufanya kazi na kampuni ya bia Tanzania TBL kutokana na mafanikio wanayo ya pata kimataifa..(Picha na Intellectuals Communications Ltd)
Akikabidhi tuzo tuzo ya dhahabu yenye hadhi ya juu zaidi ya ubora wa bidhaa kimataifa ijulikanayo kama “Grand Gold Award” Kulwa amesema kampuni yao ina mtandao wa vituo 35 ikiwemo Tanzania hivyo wanahakikisha kufikisha huduma zao kwa wakati kwenye vituo vyote ili kwenda sawa na wateja wao.

Awali akizungumza na waandishi wa habari, meneja wa Bia ya Ndovu Bi. Pamela Kikuli alisema; 
“Tunayo furaha kubwa sana kuwajulisha wadau wa Bia hii ya Ndovu Special Malt juu ya ushindi huu mkubwa ambao Bia hii imenyakua katika tuzo za bidhaa za kimataifa zinazotolewa na Taasisi ya kimataifa inayoangalia ubora wa bidhaa ya “Monde Selection International Quality Institute” iliyopo Athens, Ugiriki. Tuzo hii yenye hadhi ya juu kabisa katika ubora wa bidhaa kimataifa inajulikana kama“Grand Gold Award” na hushindanisha bidhaa toka Mataifa mbalimbali ambapo mwezi huu Aprili taasisi hiyo imetangaza rasmi kuwa “Ndovu Special Malt”imeshinda tena tuzo ya “Grand Gold” kwa mwaka 2012. Alisema Pamela.

No comments:

Post a Comment