TPBC INATAMBUA MIKATABA YA FRANCIS CHEKA NA PROMOTA KAIKE SIYAJI
Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa nchini (TPBC) inatambua mkataba (mikataba)
kati ya Francis Cheka na Kaike Siyaji aliyosaini kupigana na Japhet
Kaseba siku ya July 7, mwaka huu.
Aidha Kamisheni ya
Ngumi za Kulipwa nchini (TPBC) inamshauri bondia Francsi Cheka awe na
mawasiliano mazuri na promota wa pambano hilo ili hali ya kutoelewana
iliyokwisha kujitokeza imalizwe kwa manufaa ya tasnia ya ngumi nchini.
TPBC
inawashauri wadau wote wanaotaka kufikia makubaliano na mabondia
kutofanya hivyo nje ya utaratibu wa mchezo wa ngumi ambao ni kusaini
mikataba mbele ya Kamisheni na wakili ili maslahi ya
wote yalindwe.
Tunapenda pia kuwashauri
mabondia wote kuacha tabia ya kusaini mikataba zaidi ya mmoja hususan
wakati bado wakiwa na pambano mkononi.
No comments:
Post a Comment