Hoja ya haja kuhusu ukweli wa ukumbi wa wanahabari Bungeni Dodoma
Mpaka sasa ni wapiganaji wachache waliopo ukumbi
wa waandishi wa habari, wengine wameendelea kubanana chini na ni fujo
tu na wanachokifanya hakuna. chombo kimoja wapo 4 sasa sijui wote
wanaandika kipindi cha maswali na majibu?
Unajua
kama mtu huna historia na swala la waandishi wa Bunge ni bora
ukanyamaza, labda manyerere amesahahu swala la ukumbi wa waaandishi wa
habari Bungeni lilivyokuwa. Nimekua nikija kuandika habari Bungeni na
najua historia ya Ukumbi wa Waandishi wa Habari, Jengo hilo la kisasa
limejengwa kwa kuzingatia mahitaji ya kila mtu, waandishi wa habari
ukumbi wao upo juu na una mpaka vimeza vya kisasa vya kuwawezesha
kuandika vizuri, lakini cha kushangaza wakati wa Mhe.
Sitta akiwa Spika, mmoja wetu akaleta hoja na kutu Convince waandishi
wenzie ili tuhamishiwe gallery ya maafisa wa serikali (sehemu ambayo ni
ndogo kuliko tulipotengewa awali) kwa madai eti tuwe karibu sana na vioo
kupenyeza vimemo kwa wabunge.... tukashauriwa udogo wa eneo wenzetu
wakadai panatosha.. enzi hizo tulikuwa tukifika bungeni waandishi
takribani 15 hadi 30.
Sasa mkutano huu wa
Bunge tupo waandishi wa Habari zaidi ya 90 kutoka, kila aina ya vyombo
vya habari na blogs, na kila mmoja wetu anang'ang'ana kukaa pale chini
tulipojazana eti kuchati huku gallery ya juu ambayo ni hasa iliyo
designiwa kuwa press kukiwa empty!!! Ndio maana kelele haziishi na kila
saa watu wanapiga story badala ya kufanya kazi. leo hii madai kuwa
tunanyanyaswa sio kweli tuliyataka wenyewe na kwa kuwa kila mtu anania
yake tofauti hata uandishi wetu sasa umekuwa full magumashi tu .....
Jamani manyerere ungeuliza wakongwe kabla hajapiga picha.
Penye ukweli
tusifie jamani jengo lilijengwa kwa kukidhi mahitaji, sehemu yetu ipo
tuliikataa wenyewe…. Tusiwe domo kayaaaa jama. Kwa kuwa nipo hapa, nakuletea fotooz za ukumbi wetu na jinsi palivyo empty huku watu wamejazana hapo chini.
Mwandishi Mzalendo, Bungeni
No comments:
Post a Comment