TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Toleo la Leo
MASHINDANO YA NGOMA ZA ASILI YA BALIMI EXTRA LAGER 2012 KUTIMUA VUMBI KUANZIA JUNI 30.
Dar Es Salaam, June 25th 2012:
Kampuni
ya Bia Tanzania (TBL), kupitia bia yake ya Balimi Extra Lager, leo
imezindua rasmi mashindano ya ngoma za asili ya Balimi Extra Lager kwa
mwaka 2012. Mashindano haya ambayo yametokea kupendwa sana na wakazi wa
kanda ya ziwa yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi katika mikoa mbali mbali
ya kanda ya ziwa kuanzia Juni 30.
Akizungumza
na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi huo Jijini Dar es Salaam,
meneja wa Bia ya Balimi Extra Lager Bi. Edith Bebwa alisema; Bia ya
Balimi Extra Lager imekuwa ikiendesha mashindano haya maarufu kama
“Mashindano ya Ngoma za Asili ya Balimi Extra Lager” kwa zaidi ya miaka saba sasa , na kwa kweli napenda kusema kuwa ni mashindano yaliyotokea kupendwa sana katika kanda yetu hii ya ziwa,
Lengo
kuu la kudhamini mashindano haya ni kushirikiana na wakazi wa kanda ya
ziwa katika kuenzi na kulinda tamaduni za kanda alisema Bi Edith .
Kwa mwaka huu wa 2012, mashindano yataanza rasmi tarehe 30 Juni katika ngazi za mikoa na kumalizika tarehe 21 Julai. Tutaanza na mkoa wa Mwanza ukifuatiwa na mikoa ya Mara, Kagera, Shinyanga na Tabora, katika mpangilio ufuatao.
Tarehe
|
Mkoa
|
Viwanja
|
30/06/2012
|
KAGERA
|
Kaitaba
|
07/07/2012
|
MWANZA
|
Ccm Kirumba
|
14/07/2012
|
TABORA
|
Chipukizi
|
21/07/2012
|
SHINYANGA
|
Shycom
|
21/07/2012
|
MUSOMA
|
Bwalo la Magereza
|
28/07/2012.
|
FINALS MWANZA
|
Ccm Kirumba
|
Akielezea
juu ya zawadi za mwaka huu, bi. Edith Bebwa alisema; kama ilivyo ada ya
Bia ya Balimi, kila mwaka tumekuwa tukiongeza zawadi ili kuongeza
chachu ya ushindani na kuleta tija kwa washindani. Kwa mwaka huu
tumeongeza zawadi kwa takribani asilimia 20 ukilinganisha na mwaka jana.
Hii yote inaonesha jinsi gani bia ya Balimi inatambua, inajali na
kuthamini utamaduni wa kanda yetu. Zawadi kwa washindi ni kama
ifuatavyo;
|
Ngazi ya mkoa
|
Finali
|
Mshindi wa kwanza
|
600,000
|
1,100,000
|
Mshindi wa pili
|
500,000
|
850,000
|
Mshindi wa tatu
|
400,000
|
600,000
|
Mshindi wa nne
|
300,000
|
500,000
|
Mshindi wa tano hadi wa kumi kila kikundi
|
150,000
|
250,000
|
Pamoja
na zawadi hizi nono, pia Balimi Extra Lager itaendelea kutoa huduma
muhimu kwa vikundi shiriki kama vile chakula na malazi. Tunaamini
kabisa mambo yote haya yataongeza hamasa na msisimko katika mshindano ya
mwaka huu. Na kauli mbiu yetu kwa mwaka 2012 “Balimi Extra Lager, twajivunia utamaduni wetu”.
Akizungumzia
maandalizi ya fainali hizo, Meneja Masoko wa Tbl Fimbo Buttalah
alisema; Maandalizi yote kwa upande wetu sisi wadhamini yameshakamilika,
hivyo niwaombe tu washiriki wote ambao nimepata taarifa kuwa wamekuwa
mazoezini kwa muda sasa, waendelee na mazoezi ili kuonesha uwezo wa juu
utakaoleta ushindani na kutoa burudani yenye kiwango cha juu.
Kwa
niaba ya bia ya Balimi Extra Lager, tunapenda kuwakaribisha watu wote
kuhudhuria mashindano haya ambayo tarehe na mahali yatakapofanyikia
zitakuwa zikitangazwa redioni ili waweze kushuhudia burudani hii na
kuuenzi utamaduni wetu. Pia wananchi wasisahau kuwa katika burudani hizi
pia wataburudika na Bia yao waipendayo ya Balimi Extra lager baridi, na
kushinda zawadi mbali mbali katika promosheni za Balimi
zitakazoambatana na Mashindano haya ya Ngoma za asili ya Balimi Extra
Lager.
Kwa Maelezo zaidi wasiliana na:
Edith Bebwa, Brand Manager, +255767266410, edith.bebwa@tz.sabmiller.com
Fimbo Butallah, Marketing Manager, +255767266567, fimbo.butallah@tz.sabmiller.com
Editha Mushi, Communications & Media Manager, +255767266420, editha.mushi@tz.sabmiller.com
Kuhusu TBL
Tanzania
Breweries Limited (TBL) inatengeneza, kuuza na kusambaza bia, vinywaji
vyenye ladha ya matunda vilivyo na kilevi na vinywaji visivyo na kilevi
hapa Tanzania. TBL pia ndiyo kampuni mama ya Tanzania Distilleries
Limited pamoja na kampuni shiriki ya Mountainside Farms Limited.
Bia
zinazotengenezwa na kampuni ya TBL ni pamoja na Safari Lager,
Kilimanjaro Premium Lager, Ndovu Special Malt, Castle Lager, Vinywaji
vingine vinavyotengenezwa na kundi la makampuni ya TBL ni Konyagi Gin,
Amarula Cream, Redd’s Premium Cold na Grand Malt.
Kundi
la makampuni ya TBL limeorodheshwa kwenye Soko la Hisa la Dar es
Salaam, limeajiri watu wapatao 1,300 na linawakilishwa nchi nzima na
viwanda vinne vya bia, kiwanda kimoja cha kutoneshea, kimoja cha
kutengenezea kimea pamoja na bohari nane za kusambazia bia.
Kuhusu SABMiller
SABMiller
plc moja kati ya makampuni makubwa ya bia duniani ikiwa na mikataba ya
kutengeneza na kusambaza bia kwenye nchi zaidi ya 60 katika mabara
matano. Bia zake ni pamoja na zile za kimataifa kama Miller Genuine
Draft, Peroni Nastro Azzurro na Pilsner Urquell vilevile na bia nyingine
zinazoongoza kwenye masoko ya ndani ya nchi mbalimbali. Nje ya
Marekani, SABMiller ni moja ya kati ya makampuni makubwa yanayotengeneza
vinywaji vya Coca-Cola duniani. Hivi karibuni SABMiller plc ilinunua
kampuni ya bia ya Foster’s pamoja na shughuli zake za uzalishaji nchini
India.SABMiller imeorodheshwa kwenye masoko ya hisa ya London na Johannesburg.
No comments:
Post a Comment