**MISS UNIVERSE TANZANIA KUPATIKANA IJUMAA UKUMBI WA MAKUMBUSHO YA TAIFA DAR
Warembo
wanaotarajia kupanda jukwaani siku ya Ijumaa Wiki hii kuwania Taji la
Miss Universe 2012, wakiwa katika picha za pamoja kwenye ukumbi wa
Makumbusho ya Taifa, Posta, wakati wa mazoezi yao. Shindano hilo
litafanyika siku hiyo katika Ukumbi huo wa Makumbusho ya Taifa, mkabala
na Chuo cha IFM.
*************************************************
SHINDANO
la kumsaka mrembo wa Miss Universe Tanzania 2012, litafanyika siku ya
Ijumaa ya wiki hii ndani ya ukumbi wa Makumbusho ya Taifa uliopo Posta
jijini Dar es Salaam, mkabala na Chuo cha IFM.
Akizungumza
na mtandao huu wa www.sufianimafoto.blogspot.com, Mkurugenzi wa kampuni
ya Compass Communications, Maria Sarungi Tsehai, alisema kuwa shindano
hilo litashirikisha jumla ya warembo 20 kutoka katika mikoa mbali mbali
ya Tanzania Bara.
ambapo
aliitaja Mikoa hiyo kuwa ni pamoja na Manyara, Arusha, Dodoma, Mwanza,
Mtwara, Kilimanjaro na wenyeji Dar es Salaam na kuongeza kuwa warembo
wote wanaendelea na mazoezi chini ya wakufunzi walioboea katika masuala
ya urembo.
“Tunatarajia
kuwa na shindano lililo bora ili kuweza kumapata mrembo ambaye
ataiwakilisha nchi yetu kimataifa na kutupa sifa katika mashindano ya
kimataifa kama ilivyokuwa kwa Flaviana Matata mwaka 2007 ambapo
alishika nafasi ya saba katika mashindano yaliyofanyika nchini Mexico,”
alisema Maria.
Maria
aliwataja warembo hao kuwa ni Bahati Chando, Aisha Maulidi, Catherine
Mpulule, Cecilia Moses, Consolata Mosha, Devotha Keregese, Doris Mollel,
Doreen Mapunda na Edith Tesha.
Wengine
ni Getrude Asanterabi, Jescha Tiba, Kundi Mligwa, Lilian Kolimba, Mary
Joel, Naomi Joseph, Nyaso Malilo, Neema Mpanda, Susan Manoko, Theodora
Msenya na Winfrida Dominic.
Aliwataja
wadhamini wa shindano hilo kuwa ni Gazeti la The Citizen, gazeti dada
la Mwananchi kwa kushirikiana na wadhamini wengine, Le Grand Casino,
Urban Rose Hotel, Amina Design, Dodoma Hotel na New York Film Academy.
Aidha
Maria, alisema kuwa shindano hilo linatarajia kuanza saa 1.00 usiku
kwa warembo hao kupita jukwaani wakiwa katika aina mbalimbali za mavazi
kama vile ya ubunifu na lile la usiku.
Alisema
kuwa maandalizi kwa ajili ya shindano hilo kubwa la urembo yamekamilika
na kinachosubiliwa ni siku ya shindano ili kupata mrithi wa Miss
Universe anayemaliza muda wake, Nelly Kamwelu.
Alifafanua
kuwa wameboresha mashindano ya mwaka huu na wanatarajia kuwa na
mashindano bora kabisa tofauti na ya miaka ya nyuma.
Warembo hao wakiwa katika picha ya pozi ya pamoja.
No comments:
Post a Comment