Tuesday, June 26, 2012

ALICHOSEMA WAZIRI MKUU KUHUSU MABADILIKO YA UKUBWA WA MAGARI YA SERIKALI.


.
Waziri mkuu Mizengo Pinda leo amewasilisha bajeti ya ofisi yake kwa mwaka wa fedha 2012/2013 na kuziagiza mamlaka zote za serikali za mitaa kupitia taarifa ya mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za serikali na kuzitafutia majibu kwa lengo la kuwachukulia hatua watumishi watakaobainika kuhusika na ubadhirifu.
Pamoja na agizo hilo waziri mkuu amesema hakuna mtumishi yeyote wa serikali atakaebainika kujihusisha na matumizi mabaya ya mali za umma ambae atahamishwa kabla ya kuchukuliwa hatua za kisheria.


Prado yenye ukubwa wa injini wa CC 3000 moja ya aina ya magari yatakayotumika kwa viongozi na watendaji wakuu wa serikali.

Bajeti hiyo yenye jumla ya shilingi Trilion 3.8 kwa ajili ya matumizi ya kawaida na matumizi ya maendeleo kwa ofisi ya waziri mkuu Tamisemi na idara zake huku bilioni 113.22 zikiwa kwa ajili ya mfuko wa bunge.
Waziri Mkuu amesema “2012/2013 madiwani watalipwa viwango vipya vya posho vilivyoboreshwa, serikali inaendelea kuchukua hatua mbalimbali za kupunguza matumizi yasiyo na tija hususani ununuzi wa magari makubwa na ya kifahari ambayo gharama za ununuzi na uendeshaji ni kubwa sana”
“kuanzia 2012/2013 hatua zitachukuliwa kwa kuweka ukomo wa ukubwa wa injini za magari ambayo yanaweza kununuliwa na serikali kuu na taasisi zake pamoja na mamlaka za serikali za mitaa, chini ya utaratibu huo magari yatakayonunuliwa yatakua ni yale yasiyozidi ukubwa wa injini wa cc 3000 kwa viongozi na watendaji wakuu na yasiyozidi cc 2000 kwa watumishi wengine ambao wanastahili za kutumia magari ya serikali”


Toyota Rav 4 ina CC 2000 ni moja ya aina ya magari yenye ukubwa huo wa injini zinazohitajika.

No comments:

Post a Comment