Monday, June 25, 2012

libeneke la wanahabari bungeni Dodoma

Waandishi wa habari wanapata shida sana wakati wa kuripoti habari za Bunge. Eneo walilotengewa ni dogo, kiasi kwamba wanalazimika kuketi chini. Wanapata usumbufu mkubwa wa kuingia katika chumba hicho kwa sababu wanalazimishwa kupanda na kushuka ngazi nyingi, huku wakipita katika vyumba vingi kabla ya kugota eneo walilotengewa. Huu ni unyanyasaji ambao ofisi ya Bunge imeufumbia macho. Ukumbi ulipojengwa waandishi wa habari hawakukumbukwa kabisa. Kama inakuwa hivi kwa wanahabari, hali ikoje kwa walemavu wasiokuwa na wa kuwasemea? Picha ya mdau Manyerere Jackton, Dodoma

No comments:

Post a Comment