Deidre
Lorenz akimkabidhi picha ya Ground Zero (New York) Rais wa Mt. Kili
Marathon 1991 Onesmo Ngowi baada ya kukimbia mbio hizo.
Deidre Lorenz akiwa anahojiwa na waandishi wa Habari mjini Moshi.
Mcheza
sinema maarufu wa Marekani Deidre Lorenz ameahidi kuleta wacheza sinema
wenzake na kushiriki kwenye mbio za mwaka kesho za mt. Kilimanjaro
Marathon zitakazokuwa zinatimiza miaka 23 tangu zianzishwe mwaka 1991.
Lorenz
aliyekimbia mbio za mwaka huu ambazo zilipewa jina la “mbio za kutimiza
miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika” na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB)
amesema kuwa atakuja na timu yake ya wapiga picha ili kupiga picha
vivutio kadhaa vya Tanzania ikiwa ni pamoja na mlima Kilimanjaro. Qwiji
hili la sinema za Santorini Blue, The Great Fight, Perfect Strangers na
nyingine nyingi ameelezea kuipenda sana Tanzania.
“Sikutegemea
kuikuta nchi nzuri kama hii” alisema mcheza sinema huyo ambaye
ameshawahi kuchaguliwa zaidi ya mara 4 kugombea tuzo maarufu za Oscar.
“Sasa nimeamini kuwa mlima Kilimanjaro ni mali ya Tanzania na
nitautangaza katika sinema zangu zote”aliendelea kusema Deidre Lorenz.
Mcheza
sinema huyu ambaye ameingia kwenye mkataba na kampuni kubwa ya Google
hivi karibuni ili kuuza sinema zake katika mtandao aliielezea Tanzania
kama nchi nzuri na yenye watu wakarimu sana.
Mbio
za Mount Kilimanjaro Marathon zilianzishwa mwaka 1991 na Marie Frances
anayetoka katika jiji la matajiri la Bethesda nchini Marekani baada ya
kuombwa na balozi wa zamani wa Tanzania nchini Misri. Tangu kuanzishwa
kwake mbio hizi zimekuwa zinaleta watalii matajiri katika mji wa Moshi
kupanda mlima Kilimanjaro na kukimbia mbio hizi zinazojulikana kama
Seven Continental Races.
Hakuna masharti yote ya kukimbia mbio hizi na watanzania wanaoshiriki katika mbio hizi huwa hawatozwi pesa za kiingilio.
Kwa
kutambua mchango wake katika uchumi wake Manispaa ya Moshi
iliibadilisha jina barabara ya zamani ya Bustani Ale na kuiita Marie
Frances Boulevard ili kumuenzi mama huyu aliyejitolea maisha yake
kuutangaza mlima Kilimanjaro.
“Kila
siku napokea ujumbe kutoka nchi mbalimbali niende huko kuanzisha mbio
za marathon lakini kwa sasa basi” alisema mama huyo aliyekuwa
mtayarishaji wa vipindi vya televisheni ya ABC kabla ya kunzisha Mt.
Kilimanjaro Marathon.
Alisema
kuwa mwaka jana yeye na Rais wa klabu ya Mt. Kilimanjaro Marathon
mtanzania Onesmo Ngowi walifanya makubaliano ya Ethiopia Airlines (ET)
jijini Addis Ababa kuzifanya mbio hizo kuwa za kimataifa zaidi. “ET
walikubali kutoa ufadhili kwetu na pia kugharamia kushiriki kwetu katika
mbio za New York Marathon, Boston Marathon na Los Angelos Maratthon ili
kuitangaza vyema Tanznaia” alibainisha Frances.
Katika
makubaliano hayo, Ngowi na Frances pia wataanzisha mbio za “King
Solomon Marathon” zitakazofanyika katika jiji la Addis Ababa nchini
Ethiopia.
Deidee
Lorenz amefungua pazia kwa watu mashuhuri kushiriki katika mbio za
marathon nchini Tanzania na ni jukumu la Watanzania kuchangamkia fursa
zinazoletwa na ujio wao.
No comments:
Post a Comment