NGORONGORO HEROES KUJIPIMA KWA MISRI, RWANDA
Timu
ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes)
itacheza mechi nne za kirafiki na timu za Misri na Rwanda kabla ya
kuivaa Nigeria kwenye mashindano ya Afrika.
Ngorongoro
Heroes ambayo kwa mara ya kwanza itakuwa chini ya kocha mpya Jakob
Michelsen itaanza kwa kucheza mechi mbili za Misri zitakazofanyika Julai
3 na 5 mwaka huu, na baadaye Julai 14 na 16 mwaka huu dhidi ya Rwanda.
Mechi
zote zitachezwa nchini, na kama ilivyo Ngorongoro Heroes, Misri na
Rwanda nazo ziko kwenye kinyang’anyiro cha kusaka tiketi za kucheza
Fainali za Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 20
zitakazofanyika mwakani nchini Algeria.
Katika
raundi ya kwanza, Ngorongoro Heroes iliitoa Sudan ambapo katika raundi
ya pili imepangiwa Nigeria, na mechi ya kwanza itafanyika jijini Dar es
Salaam, Julai 29 mwaka huu. Timu hizo zitarudiana wiki mbili baadaye
nchini Nigeria.
Iwapo
Ngorongoro Heroes itafanikiwa kuitoa Nigeria, katika raundi ya mwisho
itacheza na mshindi kati ya Congo Brazzaville na Afrika Kusini.
No comments:
Post a Comment