*VYAMA VYA SIASA VINAVYOIBUKA WAKATI WA KAMPENI ZA UCHAGUZI KUFUTWA
Akizungumza
katika mahojiano na Redio One, Msajili huyo wa vyama vya Siasa nchini,
John Tendwa, alisema kuwa anatambua uwepo wa vyama vingi vya Siasa,
lakini baadhi yao vimekuwa kimya zaidi ambapo huanza kuibuka wakati wa
Kampeni na uchaguzi Mkuu.
Alisema
kuwa hivi sasa wapo katika mchakato wa kuvifuatilia vyama vyote ambavyo
haviwajibiki kwa jamii na kusubiri kujitokeza wakati wa uchaguzi na
kusema kuwa endepo vitakavyogundulika vitafutiwa usajili.
Miongoni
mwa vyama vitakavyokumbwa na kimbunga hicho ni vile visivyokuwa na
uwakilishi wa wananchi katika nganzi mbalimbali za Udiwani, Uenyekiti na
Ubunge.
No comments:
Post a Comment