KAMANDA KOVA 'ALONGA' KUHUSU KUTEKWA DKT. ULIMBOKA
Kamanda
wa polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Kamanda Suleiman Kova,
akizungumza na waandishi wa habari leo mchana kuhusu tukio la utekaji
nyara na kujeruhiwa kwa kiongozi wa mgomo wa Madaktari, Steven
Ulimboka, anayedaiwa kutekwa na watu watano wakati akipata kinwaji
katika klabu ya Leaders Kiondoni jijini Dar es salaam.
Kamanda
Kova amesema Ulimboka aliokotwa na msamaria mwema ambaye hakutaka
kumtaja jina lake kiusalama na kutoharibu upelelezi na kuwa msamaria
mwema huyo alimuokota Ulimboka katika msitu wa Mabwepande na kutoa
taarifa kituo cha polisi cha Bunju, ambapo polisi aliyekuwa zamu
alichukua maelezo yake na baadae, Steven Ulimboka, kuletwa katika
hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu zaidi.
Kamanda
Kova amesema jeshi la Polisi Kanda Maalum, limeunda jopo maalum kwa
ajili ya uchunguzi na upelelezi wa tukio hilo la utekaji nyara, kwani ni
tukio la kwanza kutoke nchini, ameongeza kwamba wahusika wote
watakaobainika kuhusika na tukio hilo watachukuliwa hatua za kisheria na
sheria itafuata mkondo wake ili kukomesha matukio mengine kama hayo.
Waandishi wa habari wakimsikilza kamanda Suleiman Kova katika kituo kikuu cha Polisi Kati jijini Dar es salaam, leo mchana.
No comments:
Post a Comment