Kampuni
ya Vodacom itakabidhi zawadi kwa washindi wa Ligi Kuu ya Vodacom msimu
2011/2012 katika hafla itakayofanyika Juni 30 mwaka huu kwenye hoteli ya
Double Tree Hilton jijini Dar es Salaam.
Hafla
hiyo itakayohudhuriwa na wawakilishi wawili kutoka katika klabu ya Ligi
Kuu itaanza saa 12 jioni. Katika hafla hiyo washindi mbalimbali
wakiwemo bingwa, makamu bingwa na mshindi wa tatu.
Wengine watakaozawadiwa ni mfungaji bora, kipa bora, timu bora yenye nidhamu, mchezaji bora wa ligi, refa bora na kocha bora.
ILALA YAENDELEA KUGAWA POINTI COPA
Ilala
imeendelea kufanya vibaya kwenye michuano ya Copa Coca-Cola baada ya
leo asubuhi (Juni 28 mwaka huu) kuchapwa mabao 4-0 na mabingwa watetezi
Kigoma katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Tanganyika Packers ulioko
Kawe, Dar es Salaam.
Mabao
yote katika mechi hiyo ya kundi A yalifungwa kipindi cha kwanza huku
Ramadhan Salum akipiga hat trick (mabao matatu). Alifunga mabao hayo
dakika ya 13, 43 na 45. Bao la pili kwa washindi lilifungwa dakika ya 19
na Athuman Rashid.
Wakati
Kigoma imeshinda mechi mbili kati ya tatu ilizocheza mpaka sasa katika
kundi hilo, Ilala imepoteza mechi zote tatu ilizocheza. Ilala imefungwa
na Arusha, Kigoma na Lindi wakati mechi yake inayofuata itakuwa Juni 30
mwaka huu dhidi ya Kusini Pemba.
Nayo
Kilimanjaro imeendelea kufanya vizuri katika kundi lake la D baada ya
leo asubuhi (Juni 28 mwaka huu) kuitandika Shinyanga mabao 3-0 kwenye
Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam.
Mabao
ya Kilimanjaro ambayo hadi sasa imeshinda mechi mbili na kutoka sare
moja yalifungwa na Adam Soba dakika ya 11 na 46 wakati la tatu
lilifungwa dakika ya 81 na James Henry.
Katika
mechi nyingine zilizochezwa leo asubuhi (Juni 28 mwaka huu), Temeke na
Mtwara zilitoka sare ya bao 1-1 kwenye Uwanja wa Tamco mkoani Pwani. Ali
Makalani alianza kuifungia Temeke na baadaye Adam swaleh akaisawazishia
Mtwara.
Uwanja
wa Nyumbu mkoani Pwani ulishuhudia Morogoro na Kaskazini Pemba zikitoka
sare ya bao 1-0. Amin Kassim aliifungia Kaskazini Pemba dakika ya 51,
na Morogoro wakasawazisha dakika ya 75 kupitia kwa Mutalemwa Katunzi
katika mechi hiyo ya kundi B.
Mechi
zitakazochezwa leo jioni (Juni 28 mwaka huu) ni Lindi vs Arusha
(Tanganyika Packers), Manyara vs Mjini Magharibi (Nyumbu), Kinondoni vs
Mbeya (Tamco) na Kusini Unguja vs Pwani (Karume).
Kesho (Juni 29 mwaka huu) ni mapumziko, na michuano hiyo itaendelea tena Juni 30 mwaka huu kwenye viwanja vyote vinne.
No comments:
Post a Comment