WAANDISHI WASIO NA AJIRA WACHAGUA VIONGOZI WAO
Viongozi
wa Chama Cha Waandishi wa Habari wasio na ajira Tanzania (TCJ) wakiwa
katika picha ya pamoja na viongozi wao mara baada ya uchaguzi
uliofanyika katika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO)
CHAMA
cha Waandishi wa Habari wasio na Ajira Nchini (TCJ) leo asubuhi
kimefanya uchaguzi na kupata viongozi wake katika ngazi mbalimbali kwa
lengo la kukiimarisha chama hicho.
Katika
uchaguzi huo Mobin Sarya anaendelea na nafasi yake ya Uenyekiti, huku
nafasi ya Makamu Mwenyekiti ikishikiliwa na Asha Bani aliyemuangusha
mpinzani wake Suleiman Msuya, huku Katibu Mkuu akiwa Samson Fredon na msaidizi ni Mpina Balile.
Nafasi ya Mweka hazina amechaguliwa Ratifa Baranyikwa ambaye hakuwa na mpinzani huku msaidizi wake akiwa Shehe Semtawa .Kamati ya Nidhamu amechaguliwa Darlin Said,Marietha Mkoka na StellaMushi.
Kamati ya Uchumi na Mipango ni Nasra Abdallah,Avitus Chami, Ratifa Baranyikwa ambaye ni mweka hazina na Shehe Semtawa.
Kamati yote imeahidi kufanya kazi kwa kushirikiana ili kuweza kufikia malengo yaliyowekwa.
Awali
kabla ya kufanyika kwa uchaguzi huo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Idara
Habari (MAELEZO), Clarence Nanyaro, alisema anafahamu wanahabari
wanavyopata shida ya kusota kwa muda mrefu bila kuajiriwa kutokana na
kutokuwa na sheria ya kuwalinda hivyo ni vyema kuwa na umoja wa kudai
sheria ya Habari.
“Ni vyema mkatumia chama hicho katika kudai haki zenu mpate nafasi kumpata waziri husika ili muweze kumuelezea
matatizo na changamoto ambazo zinawakabili wanahabari kwa kuweka
mikakati na sheria zitakazosaidia hata kuweza kudai haki zenu,”alisema .
Chama cha TSJ kilianzishwa mwaka 2008 na kupata usajili rasmi mwaka 2011 katika Wizara ya Mambo ya Ndani kama chama cha waandishi.
No comments:
Post a Comment