Tuesday, June 26, 2012

Shule ya sekondari ya Olasiti yakabidhiwa msaada wenye thamani ya shilingi milion 7

SHULE ya sekondari ya Olasiti iliyopo katika kata hiyo  jijini Arusha,
imeondokana na changamoto kubwa iliyokuwa ikiwakabili kwa kipindi cha
muda mrefu ya ukosefu wa madawati iliyosababisha wanafunzi kukalia ndoo
na mawe, hali ambayo iliwalazimu  wadau mbalimbali wa elimu kujitokeza
nakusaidia  viti mia mbili na meza zake.

Msaada huo umetolewa hivi karibuni na Alex Martin ambaye
ni mfanyabiashara wa jijini hapa na kuukabidhi kwa uongozi wa kata hiyo
(ODC)mbele ya  mkuu wa shule hiyo,Paulina Alex Bagoye ambapo msaada huo
umeweza kupunguza changamoto kubwa iliyokuwaikiwakabili wanafunzi wa
shule hiyo kwa muda mrefu.

Akizungumza wakati wa kukabithi msaada huo, Mfanyabiashara huyo,
alisema kuwa alifikia hatua ya kutoa meza na viti mia moja  ambavyo
vina thamani ya  shs  7milioni kwa shule hiyo ambapo awamu ya kwanza
aliwahi kusaidia viti nameza  hamsini vyenye thamani ya shs  3.5
milioni huku lengo likiwa ni kuwawezeshawanafunzi kuweza kusoma katika
mazingira mazuri na hatimaye kuongeza ufaulu wa masomo.

Alisema kuwa, shule hiyo imekuwa ikikabiliwa na changamotohiyo
kutokana na upya kwani kabla ya hapo kata hiyo ilikuwa haina shule
yasekondari hali ambayo ilikuwa ikiwalazimu  wanafunzi kutembea umbali
mrefu wa zaidi yakilometa  kumi na tano kufuata elimu yasekondari
katika shule ya Oljoro iliyopo kata ya Terat jijiji hapa.

Aliongeza kuwa, hatua ya wanafunzi hao kusoma wakikalia ndoona mawe
imekuwa ikichangia kwa kiasi kikubwa sana kutofanya vizuri kimasomo
kwawanafunzi hao kwani walikuwa wakisoma katika mazingira magumu sana,
hivyo halihiyo ilimlazimu kutafuta jitihada mbalimbali kwa
kuwashirikisha marafiki nawadau mbalimbali katika kumuunga mkono
kuisaidia shule hiyo.

‘’Kwa kweli shule hii inakabiliwa na changamoto nyingi sanakwani ndo
kwanza ina kidato cha kwanza ,hivyo juhudi za haraka
zinahitajikakatika kuhakikisha tunaongeza madarasa mengine ili mwakani
wanafunzi wenginewaweze kusoma,huku lengo langu likiwa ni kutoa jumla
ya madawati mia mbilipamoja na meza zake ‘’alisema Martin.

Naye Mkuu wa shule hiyo, Paulina Alex Bagoye alisema kuwa,msaada huo
umesaidia kupunguza changamoto ya wanafunzi hao kukalia ndoo na mawe,
ambapo kabla ya kupata msaada  huo wamadawati mia na hamsini jumla ya
wanafunzi sitini na moja walikuwa hawana madawati,hivyo kupitia msaada
huo umepunguza kwa kiasi kikubwa sana changamoto hiyo.

Alitaja changamoto nyingine inayowakabili kuwa ni pamoja naukosefu wa
nyumba za waalimu ambapo walimu wamekuwa wakipanga uraiani,ukosefuwa
samani za ofisi ,pamoja  na ukosefu wachoo cha walimu huku walimu
wakiendelea kuchangia choo na wanafunzi hali ambayoni hatari sana .

Alitoa wito kwa wadau mbalimbali kuiga mfano wamfanyabaishara huyo
katika kujitokeza kwa wingi kuisaidia shule hiyo ambayoinakabiliwa na
changamoto nyingi sana ,na kwa kufanya hivyo itasaidia kuongezakiwango
cha ufaulu kwa wanafunzi walio wengi shuleni hapo.

No comments:

Post a Comment