HIVI ULISIKIA ALICHOSEMA WAZIRI MKUU BUNGENI? KUHUSU KUJIUZULU NA MGOMO WA MADAKTARI? CHOTE KIKO HAPA..
Leo ndio siku ambayo waziri
mkuu Mizengo Pinda aliahidi kutoa jibu la serikali bungeni kuhusu
itakachofanya kuhusu mgomo wa Madaktari.
Kuhusu kujiuzulu kutokana na
mgomo wa sasa likiwa ni swali kutoka kwa mbunge Tundu Lisu wa Singida
Mashariki amesema “yako mazingira unaweza ukawajibika kwa njia hiyo
lakini sio lazima yakawa yoote na mimi sioni kama hili ni moja ya maeneo
ambayo unaweza ukasema kistahiki hivi unaweza kufikia hatua hiyo,
ninachokubali tu ni kwamba tatizo hili ni kweli ni la muda mrefu na
nimefanya kila njia kujaribu kulitatua kwa kiasi kikubwa sana, inabidi
tukubali kwamba bado lina changamoto nyingi kwa sababu ya mambo mengi tu
ambayo yameingiliana na mgogoro wenyewe”
Freeman Mbowe kiongozi wa kambi
ya Upinzani bungeni alisimama na kumuuliza Waziri Mkuu kwamba “ulitoa
kauli ambayo kama mzazi au kama baba imetia hofu kubwa sana katika taifa
pale ulipokua unazungumzia mgomo wa Madaktari na hatimae ukasema na
LITAKALOKUWA NA LIWE, vilevile zilipatikana taarifa nyingine kwamba rais
wa Madaktari ametekwa juzi usiku, ameteswa, kavunjwa meno, kango’lewa
kucha.. unalieleza nini taifa kuhusu kauli yako ya LITAKALOKUA NA LIWE?
na serikali inafanya nini cha ziada?
Hili ndio jibu alilotoa Waziri
mkuu kwa Freeman Mbowe: “Kwanza nikiri kwamba ni kweli nilitamka hivyo
jana lakini kilichokua kinanisumbua kichwani ni kwa sababu nilijua jambo
hili liko mbele ya mahakama kuu, kuhusu yaliyompata Dr Ulimboka
naonyesha masikitiko yangu juu ya jambo hili na ninamtakia kila la kheri
na apone haraka”
Kuhusu alichoahidi kukiongea
leo kuhusu Mgomo unaoendelea Waziri Mkuu amesema “tumezungumza na vyombo
mbalimbali ili tuone katika mazingira tuliyonayo ni namna gani
tutawahudumia wagonjwa, tumewaomba wenzetu wa LUGALO tutumie hospitali
ile kuhakikisha wagonjwa hawakosi hiyo huduma, hata hospitali zake
nyingine ndogo zote tumeamue tuzitumie kwa njia hiyo, lakini pia tumeona
ni vizuri kama kutakua na madaktari wengine waliostaafu na wengine
waliopo wizarani pale wote tumeomba sasa watafutiwe njia mbalimbali ili
warudi waweze kutoa hiyo huduma kwa Watanzania”
No comments:
Post a Comment