(JUMIKI) imepinga uvumi uliosambazwa nchini kuwa leo kutakuwa na maandamano ya Jumuiya hiyo
Na Ali Issa-Maelezo Zanzibar
Jumuiya
Ya Uamsho Na Mihadhara Ya Kiislamu (JUMIKI) imepinga uvumi uliosambazwa
nchini kuwa leo kutakuwa na maandamano ya Jumuiya hiyo na kudai kuwa
propaganda hizo zinaendeshwa na baadhi ya watendaji katika jeshi la
polisi na usalama wa taifa ambao hawaitakii mema Jumuiya yao.
Hayo
yamesemwa na Amiri wa Jumuiya hiyo Sheikh Farid Ahmed wakati alipokuwa
akizungumza na Waandishi wa Habari katika Ukumbi wa Habari Maelezo
Zanzíbar kuhusiana na tuhuma ambazo wamezitoa kwa Jeshi la Polisi dhidi
ya Jumuiya yao.
Amedai
kuwa Jumuiya haijapanga maandamano kwani ni taasisi inayofanya kazi
zake kisheria nakwamba hata ikitokezea kufanya maandamano basi watafuata
taratibu zote za kisheria ikiwa ni pamoja na kulitaarifu rasmi Jeshi la
Polisi.
Aidha
amedai kuwa kuna mkakati wa muda mrefu wa kutaka kuwabatiza viongozi
wakuu wa jumuiya hiyo kesi za ugaidi hususan Amir Mkuu wa jumuiya ya
Maimamu Zanzibar Sheikh Farid Hadi Ahmed ili kuzima vuguvugu la kudai
Zanzibar huru.
Shekh
Faridi amedai kuwa inasemekana kuna mahusiano makubwa baina ya
watendaji ndani ya Jeshi la polisi pamoja na baadhi ya wageni
wanaosadikiwa kuwa ni raia wa Marekani juu ya kuutekeleza mkakati huo
baada ya kuwa tayari umeshakamilika.
Amedai kuwa kuna ukiukwaji mkubwa wa haki za kirai ambao umekuwa ukifanywa na Jeshi la Polisi Zanzibar kwa kuwanyima haki ya kufanya mihadhara yao ndani ya Misikiti ambapo Juni 17 mwaka huu wananchi mbalimbali walijeruhiwa kwa mabomu katika vijiji vya Donge,Mkwajuni na Mahonda.
Ameliomba
Jeshi la Polisi kufanya kazi zake za kulinda usalama wa wananchi na
mali zao na kuacha kufanya kinyume chake kwani huko ni kuchochea chuki
kati ya Jeshi hilo na raia.
Amesisitiza
haja ya wazanzibari kuungana na kuachana na Itikadi zao za kivyama
katika kudai hadhi ya Rais na mamlaka ya Nchi ya Zanzibar ndani na nje
ya Zanzibar pale tume ya mabadiliko ya Katiba itakapoanza kazi zake.
Kwa
upande wake Naibu Naibu Amir Jumuiya Ya Uamsho Na Mihadhara Ya Kiisilam
Sheikh, Azan Khalid Hamdan amewaomba wanahabari nao kuwa makini katika
taaluma yao kwa kufanya usawa wa taarifa ambazo wamekuwa wakizitoa.
Hivi
karibuni Jumuiya hiyo ilitangaza rasmi kushiriki kikamilifu katika
zoezi zima la kutoa maoni yao katika mchakato wa kupata Katiba mpya ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kubadili msimamo wao wa awali wa
kuisusia Tume hiyo.
No comments:
Post a Comment